Njia ya Mkojo Kuziba

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Je, kuziba kwa njia ya mkojo ni nini?

Njia yako ya mkojo ni njia ambayo mkojo hufuata kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu chako cha mkojo na kutoka mwilini. Kuziba inamaanisha njia yako ya mkojo ina kizuizi sehemu fulani katika njia hiyo.

  • Kuziba kwa njia ya mkojo kunaweza kutokea kwenye figo zako, kwenye bomba ambazo zinaunganisha kila figo kwenye kibofu chako cha mkojo (ureta), kibofu chako cha mkojo, au bomba ambalo mkojo wako hupita ili kutoka nje (urethra)

  • vitu vingi vinaweza kusababisha kuziba kwa njia ya mkojo, ikijumuisha makovu ya tishu, uvimbe, au mawe kwenye figo

  • Kuziba kwa njia ya mkojo kunaweza kusababisha maumivu na maambukizi

  • Hali hii ikiendelea kwa muda wa kutosha, kuziba kwa njia ya mkojo kunaweza kusababisha uharibifu wa figo

  • Madaktari huondoa kizuizi kwa kutumia dawa au upasuaji kwa kutegemea chanzo chake

Figo Iliyovimba

Kwenye hidronefrosisi, figo huvimba (hutanuka) kwa sababu mtiririko wa mkujo umezuiwa. Mkojo hurejea nyuma ya kizuizi na kubakia kwenye bomba ndogo za figo na eneo la kati la ukusanyaji (pelvis ya figo).

Je, nini husababisha kuziba kwa njia ya mkojo?

Sababu za kawaida za kuziba kwa njia ya mkojo ni pamoja na:

Sababu nyingine za kuziba kwa njia ya mkojo ni pamoja na:

  • Tishu yenye kovu kutokana na tiba ya mionzi, upasuaji au utaratibu wa kimatibabu

  • Kuota vinyama vyenye saratani au visivyo na kansa (sio hatarishi)

  • Damu iliyoganda

Zipi ni dalili za kuziba kwa njia ya mkojo?

Dalili za kuziba kwa njia ya mkojo zinategemea sehemu kilipo kizuizi, kasi ya kutokea hali hiyo, na kizuizi ni kibaya kwa kiasi gani.

Dalili zinajumuisha:

  • Maumivu makali upande mmoja wa tumbo lako au upande mmoja wa mgongo wako chini ya mbavu

  • Kupungua kwa kutiririka kwa mkojo

  • Kukojoa sana usiku

  • Kichefuchefu na kutapika

Unaweza kupata homa na usaha au damu kwenye mkojo wako, iwapo kizuizi kitasababisha maambukizi ya njia ya mkojo.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kizuizi cha njia ya mkojo?

Madaktari hushuku uwepo wa kizuizi cha njia ya mkojo kutokana na dalili zako. Ili kuwa na uhakika kwa kawaida watafanya:

  • Uchunguzi wa upigaji picha kwa mawimbi ya sauti au CT (tomografia ya kompyuta).

Ikiwa itaonyesha uwepo wa kizuizi lakini pasipo chanzo, madaktari wanaweza:

  • Kufanya sistourethrografia ya kuacha kibofu kikiwa kitupu (VCUG), kipimo ambapo madaktari huingiza rangi katika kibofu chako cha mkojo kwa kutumia katheta na kupiga eksirei kuona mtiririko wa mkojo

  • Kutumia mpira wa kuangalia unaoweza kupinda ili kukagua mrija wa mkojo, tezi dume na kibofu chako cha mkojo

Madaktari wanaweza pia kufanya vipimo vya damu kutafuta dalili za kuharibika kwa figo na vipimo vya mkojo kutafuta maambukizi ya njia ya mkojo.

Je, mdaktari hutibu vipi kizuizi cha njia ya mkojo?

Madaktari wataondoa kizuizi kutoka kwenye njia ya mkojo.

  • Ikiwa una jiwe kwenye figo, kwa kawaida madaktari watasubiri lipite lenyewe

  • Iwapo jiwe la figo halitapita lenyewe, madaktari watajaribu kulivunja kwa kutumia mawimbi makali ya sauti (lithotripsi ya mtetemo wa mawimbi) au kuondoa jiwe hilo kwa kutumia skopu.

  • Kwa tezi dume iliyotanuka, madaktari watakupatia dawa au homoni za kupunguza ukubwa wa tezi dume

  • ikiwa hawawezi kuondoa kizuizi, madaktari wataingiza bomba ndani ya figo yako ili kutoa mkojo

Madaktari pia watatibu tatizo lolote ambalo limesababishwa na kizuizi cha njia ya mkojo, kama vile maambukizi ya njia ya mkojo au tatizo la figo.