Haipaplasia ya Kuvimba kwa Tezi Dume (BHP)

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2023

Je, tezi dume ni nini?

Tezi dume ni tezi inayopatikana kati ya kibofu cha mkojo na uume. Mrija wa mkojo (urethra) unaobeba mkojo kutoka kwenye kibofu hadi nje ya uume unapita katikati tezi kibofu.

Tezi dume hutengeneza majimaji ambayo hulinda shahawa. Karibu majimaji yote ambayo humtoka mwanaume wakati wa kujamiiana hutengenezwa na tezi dume.

Kwa vijana, tezi dume inatoshana na karanga lakini ukubwa wake huongezeka kadri unavyozidi umri.

BPH ni nini?

BPH ni wakati tezi dume yako inakua kiukubwa, lakini ukuaji huo si saratani. BPH inaweza kuifanya ngumu kukojoa (kutoa mkojo), kwa sababu tezi dume iliyoongezeka kwa ukubwa inaweza kufinya neli ambayo hubeba mkojo (mrija wa mkojo)

  • BPH hutokea kwa sana baada ya umri wa miaka 50

  • Madaktari hutambua BPH kwa kuingiza kidole chenye glavu kwenye rektamu yako (mwisho wa njia yako ya mmeng'enyo wa chakula mahali kinyesi [haja kubwa] huhifadhiwa) na kuhisi tezi dume hio (uchunguzi wa rektamu)

  • Unaweza kufanyiwa vipimo ili kuangalia jinsi ambavyo mkojo wako unatiririka na vipimo vingine ili kuhakikisha kuwa hauna saratani ya tezi dume

  • Unaweza kosa kuhitaji matibabu ya BPH

  • Ikiwa dalili zako zinakusumbua sana, unaweza kuhitaji kutumia dawa au kufanyiwa upasuaji

Je, ni nini kinachosababisha BPH?

Madaktari hawana uhakika ni nini husababisha BPH. Kuna uwezekano ni kwa sababu ya mabadiliko katika homoni unapozeeka.

Dalili za BPH ni zipi?

BPH huzuia mtiririko wa mkojo, kwa hivyo wanaume wanaweza kupata dalili hizi:

  • Kutatizika kuanza kukojoa

  • Kuwa na mtiririko mdogo na hafifu wa mkojo

  • Kubakia kwa matone ya mkojo katika kumalizia kukojoa

Kwa sababu mtiririko wa mkojo umezuiwa, kibofu chako cha mkojo hakimalizi mkojo kabisa na unaweza:

  • Kuhisi kama kukojoa hakujakamilika

  • Kuhitaji kukojoa mara nyingi, haswa usiku

  • Kuhisi hitaji la haraka la kukojoa

  • Kupata maambukizi ya kibofu cha mkojo

Wakati mwingine mtiririko wa mkojo umezuiwa kabisa kwa hivyo huwezi kojoa hata kidogo (hali ambayo madaktari wanaita uhifadhi wa papo hapo wa mkojo). Wakati hili linafanyika, kibofu chako cha mkojo hujaa mkojo kwa haraka na huwa na maumivu makali sana. Itakuwa kuwa na uchungu mkubwa utataka na kuhitaji kuona daktari mara moja.

What Happens When the Prostate Gland Enlarges?

In benign prostatic hyperplasia, the prostate gland enlarges. Normally the size of a walnut, the prostate gland may become as large as a tennis ball. The enlarging prostate gland squeezes the urethra, which carries urine out of the body. As a result, urine may flow through more slowly.

Madaktari wanawezaje kujua kama nina BPH?

Daktari wako atauliza kuhusu dalili zako na kufanya uchunguzi wa rektamu:

  • Daktari huvalia glavu na kuingiza kidole kwenye rektamu yako (mwishoni mwa njia yako ya mmeng'enyo wa chakula ambapo kinyesi [haja kubwa] huhifadhiwa)

  • Daktari wako anaweza kuhisi tezi dume yako wakati wa uchunguzi

  • Ikiwa uan BPH, daktari atahisi tezi dume yako ikiwa kubwa na laini

Ikiwa unakumbana na matatizo mengi unapokojoa, daktari wako anaweza kufanya kipimo cha uroflowmetry. Katika kipimo hiki, unakojolea kifaa ambacho kinapima kiwango cha mkojo na kasi ambayo unatiririka nayo. Baada ya kipimo cha mtiririko wa mkojo, madaktari watapiga picha ya mawimbi ya sauti ili kuona kibofu chako kilitoa mkojo kiasi gani. Picha ya mawimbi ya sauti hutumia mawimbi ya sauti kupima kiwango halisi cha mkojo ndani ya kibofu chako cha mkojo.

Saratani ya tezi dume pia hufanya tezi dume iwe kubwa zaidi. Madaktari wanahitaji kujua iwapo dalili zako ni za BPH au saratani ya tezi dume. Wakati mwingine saratani hutengeneza uvimbe ambao daktari anaweza kuhisi kwenye tezi dume yako lakini mara nyingi haitengenezi uvimbe. Kwa hivyo kwa kawaida, daktari:

  • Hafanya kipimo cha damu kinachoitwa kiwango cha PSA (kiwango cha antijeni mahususi kwa tezi dume)

Kulingana na kiwango cha PSA, uchunguzi wako na vitu vingine, daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe:

  • Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi wa tezi dume

Kwa uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi wa tezi dume, daktari hutumia sindano yenye shimo kuchukua sampuli za tishu kutoka kwenye tezi dume yako. Kwanza, daktari huweka kipima kidonda cha upigaji picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwenye rektamu. Picha za upigaji picha kwa kutumia mawimbi ya sauti huonyesha daktari mle pa kuelekeza sindano. Kwanza daktari huchoma sindano ya dawa ya kutia ganzi na kisha huchukua sampuli kadhaa.

Madaktari hutibu vipi BPH?

Kwa kawaida madaktari huwa hawatibu BPH isipokuwa kama dalili zinakusumbua au kusababisha maambukizi. Kama matukio kama hayo, daktari wako anaweza kukupatia dawa.

Baadhi ya dawa hutuliza sehemu fulani za tezi dume na kibofu cha mkojo ili kuimarisha mtiririko wa mkojo. Dawa zingine hupunguza ukubwa wa tezi dume. Dawa zisipofanya kazi, unaweza kuhitaji upasuaji.

Kwenye upasuaji, unaoitwa TURP ambayo inasimamia transurethral resection of the prostate (upasuaji wa kutoa sehemu ya ndani ya tezi dume), daktari:

  • Huweka skopu kwenye uume wako hadi kwenye tezi dume

  • Hutumia vifaa au leza kuondoa sehemu ya tezi dume

Mara nyingi, utaratibu wa TURP utatuliza dalili zako. Lakini kuna hatari kidogo utadondokwa na mkojo baadaye au kuwa na tatizo kuamsha uume.

Ukipata mshtuko wa ghafla ambapo hauwezi kukojoa hata kidogo (uhifadhi wa mkojo wa papo hapo), utahitaji katheta. Katheta ni neli ya mpira ambayo daktari huweka kupitia kwenye uume wako na kwenye kibofu cha mkojo. Katheta hutoa mkojo nje. Kwa kawaida utahitaji kuweka katheta ndani kwa siku kadhaa.