Je, polio ni nini?
Polio ni maambukizi ya virusi ambayo huathiri neva zinazodhibiti misuli.
Polio husambaa pale watu wanapokula chakula chenye maambukizi, au maji au kugusa sehemu iliyo na maambukizi na kisha kugusa midomo yao
Watu wengi huwa na dalili za kawaida, kama vile kichwa kuuma na vidonda kwenye koo, na huwa hata hawafahamu kuwa wana polio
Kwa watu wachache, polio husababisha hali ya udhaifu na kupooza misuli moja kwa moja (kushindwa kusogeza sehemu ya mwili wako)
Pia polio husambaa kupitia kinyesi, mate au chafya kutoka wka watu wenye maambukizi
Chanjo ya polio (sindano) huzuia polio
Je, nini husababisha polio?
Polio husababishwa na kirusi cha polio. Inaambukizwa kwa urahisi na husambaa kwa kugusana na watu wenye maambukizi.
Polio ilikuwa imesambaa sehemu kubwa ya dunia hadi miaka ya 1950, pale chanjo ilipopatikana. Tukio la mwisho la uwepo wa polio nchini Marekani lilikuwa mwaka 1979. Bado watu hupata polio katika maeneo ya Afrika (Hasa Naijeria), Pakstani, na Afghanistani.
Je, dalili za polio ni zipi?
Watu wengi huwa hawana dalili zozote. Ikiwa una dalili, kwa kawaida huwa ni za kawaida, kama vile homa, koo lenye vidonda, na maumivu ya kichwa kiasi. Kwa sababu watu hawaumwi sana, mara nyingi madaktari huwa hawafanyi vipimo vyovyote na hata ugonjwa huwa hautambuliwi kama polio.
Ni watu wachache ambao hupata dalili kali:
Maumivu makali ya kichwa
Shingo na mgongo mgumu
Maumivu ya misuli
Baadhi ya watu wenye dalili kali zaidi huwa na matatizo mabaya:
Udhaifu wa misuli ambao unaweza kudumu kwa muda mrefu
Kupooza, hali inayokufanya ushindwe kusogeza sehemu ya mwili wako
Kupooza kunaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili wako. Unaweza kushindwa kusogeza mguu mmoja au yote miwili. Unaweza kushindwa kumeza au hata kupumua.
Je, madaktari wanawezaje kufahamu ikiwa nina polio?
Madaktari hushuku kuwa una polio kwa kutegemea dalili zako na kama umekuwa katika eneo ambalo watu wengine wana polio. Ili kuwa na uhakika, watafanya:
Fanya vipimo vya damu
Vipimo vya sampuli za kinyesi chako au koo
Watafyonza majimaji ya uti wa mgongo ili kupima majimaji hayo
Je, madaktari hutibu vipi polio?
Hakuna tiba ya polio. Madaktari watafanya:
Watakufanya utumie dawa ili kupunguza maumivu na homa
Iwapo huwezi kupumua, wanaweza kukuweka kwenye mashine ya upumuaji (mashine ya kukusaidia kupumua)
Watu wenye dalili kiasi za polio mara nyingi hupona kabisa. Watu wenye polio kali mara nyingi hupata udhaifu wa misuli kwa muda mrefu. Wakati mwingine, hata kama dalili zitapungua au kupotea, udhaifu wa misuli unaweza kuongezeka au kurejea baada ya miaka mingi baadaye (ugonjwa wa baada ya polio)
Je, ninawezaje kuzuia polio?
Pata chanjo ya kirusi cha polio, ambayo imejumuishwa kwenye ratiba ya chanjo za watoto.
Nchini Marekani, watoto hupata chanjo wakiwa na umri wa miezi 2, miezi 4, miezi 6 hadi 18, na miaka 4 hadi 6
Iwapo hukupata chanjo zote za chanjo ya polio utotoni, zungumza na daktari wako kuhusu kupata chanjo ukiwa mtu mzima.
Iwapo unasafiri kwenda katika eneo lenye polio, zungumza na daktari wako kuhusu kama unatakiwa kuchoma chanjo nyingine hata kama ulichoma chanjo hapo kabla