Maumivu ya macho

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Maumivu ya macho yanaweza kuwa makali, kuuma au uchungu wa mdundo. Unaweza kuhisi kama kuna kitu machoni mwako.

Pamoja na uchungu, unaweza kuwa na wekundu wa macho au dalili zingine, kama vile uoni hafifu au jicho linalovimba. Uchungu unaohisi unaweza kuwa mkali sana wakati uko kwenye mwangaza angavu.

Ni nini husababisha uchungu kwenye macho?

Visababishaji vya kawaida zaidi vya uchungu kwenye macho ni matatizo kwenye konea yako. Konea yako ni safu ya wazi mbele ya jicho lako. Ina hisia za uchungu.

Visababishaji vya kawaida zaidi vya uchungu kwenye macho ni:

  • Konea iliyoambukizwa au iliyokunwa

  • Kitu machoni mwako

Matatizo mengine ya macho ambayo yanasababisha uchungu yanajumuisha:

  • Glaukoma—shinikizo la juu ndani ya jicho lako

  • Contact lens keratitis—tatizo linalosababishwa na kuvalia lensi zako zinazogusa kwa muda mrefu zaidi

  • Jicho la rangi ya waridi

  • Herpesi zoster ophthalmicus—maambukizi ya mbwe ambayo huathiri jicho lako

  • Maambukizi ndani ya jicho—haya ni ya kawaida zaidi ikiwa hivi karibuni ulifanyiwa upasuaji wa jicho au ulipata jeraha kwenye macho

  • Kuvimba kwa neva ya optiki (ugonjwa wa neva ya optiki)—uchungu kidogo ambao unauma wakati jicho linasonga

Matatizo katika sehemu zingine za mwili wako yanaweza pia kusababisha uchungu kwenye macho, kama vile:

Ni lini ninapaswa kuona daktari kuhusu uchungu kwenye macho?

Ona daktari mara moja ikiwa una uchungu mwingi sana kwenye macho au uchungu kwenye macho pamoja na yoyote ya ishara hizi za onyo:

  • Kutapika

  • Jicho jekundu

  • Kuona duara za mwangaza karibu na taa

  • Homa, mzizimo, uchovu au uchungu kwenye misuli

  • Kutoweza kuona dhahiri kama kawaid (udhahiri kiasi)

  • Jicho lililofura

  • Kushindwa kusogeza jicho lako kwa kila upande (kulia, kushoto, juu na chini)

Uchungu mkali kwenye macho unaweza kusababisha kupotea kwa uwezo wa kuona. Nenda kwa daktari mara moja—usisubiri.

Ikiwa una uchungu kiasi kwenye macho bila ishara za onyo au ukihisi kama kuna kitu kwenye macho yako, uchungu kwenye macho yako si mkali kwa kawaida. Unaweza kusubiri siku moja au 2 uchungu wako ukiisha wenyewe. Usipoisha, nenda kwa daktari.

Je, nitarajie nini ninapokwenda kumwona daktari wangu?

Madaktari watauliza maswali kuhusu dalili zako na kuangalia macho na kope zako. Kwa kawaida, daktari hufanya yafuatayo:

  • Kukagua uwezo wako wa kuona kwa kutumia chati ya macho

  • Kuweka matone ya kioevu kwenye jicho lako (huenda ukahisi mwasho kwa sekunde chache)

  • Kuangalia ndani ya jicho lako kwa kutumia mwanga maalum wa lenzi (mwangaza mkali sana)

  • Kupima shinikizo kwenye jicho lako (kuna njia tofauti za kufanya hivyo, lakini hamna inayoumiza)

Endapo daktari anaamini kuwa kuna kitu kwenye jicho lako, huenda akageuza kope zako nje kwa muda mfupi ili kuangalia jicho lako kwa karibu zaidi. Huenda ukahisi usumbufu usio wa kawaida, lakini hutahisi uchungu. Huenda ukapimwa damu au ukafanyiwa eksirei ikiwa daktari anaamini kuwa inawezekana mboni ya jicho lako imepata maambukizi.

Madaktari wanatibu vipi uchungu kwenye macho?

Madaktari watatibu kisababishaji cha uchungu kwenye macho yako. Kwa mfano, watakupa dawa ikiwa una maambukizi.

Unaweza kuhitaji kutumia dawa za kuandikiwa na daktari au vituliza uchungu vya kununua hadi uchungu uishe. Hata kama kuna dawa ambazo zinaweza kutia ganzi macho yako kwa muda mfupi, madaktari hawapendi wewe ukitumia hizi nyumbani. Hio ni kwa sababu jicho lako likitiwa ganzi, hautaweza kujua kama tatizo lako linakuwa mbaya zaidi.