Retinopethia ya Kisukari

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Retina ni safu ya seli nyuma ya jicho lako ambayo hutambua mwangaza na kutuma mawimbi kwenye ubongo ili kukuwezesha kuona.

Retina inalishwa na mishipa midogo mingi ya damu. Mishipa ya damu inaweza kuharibika kwa watu wenye kisukari. Mishipa hii inaweza kuvujisha damu na kuharibu retina. Wakati mwingine mishipa iliyoharibiwa inaweza kurejea ikiwa na matatizo, jambo linaloweza kufanya tatizo liwe baya zaidi.

Retinopethia ya kisukari ni nini?

Retinopethia ya kisukari ni uharibifu kwenye retina yako unaosababishwa na kuwa na kisukari. Watu wenye kisukari wana viwango vya juu vya sukari kwenye damu. Sukari nyingi kwenye damu inaharibu mishipa ya damu. Mishipa midogo ya damu kwenye figo na kwenye jicho ipo katika hatari ya kuharibika.

  • Kila mtu mwenye kisukari anakuwa na mabadiliko fulani kwenye retina yake

  • Unaweza ukawa na retinopethia ya kisukari na usijue

  • Ikiwa retinopethia ya kisukari inakuwa mbaya zaidi, unaweza kupata matatizo ya uoni wako

  • Madaktari wanatibu retinopethia ya kisukari kwa kutumia matibabu ya leza na sindano kwenye jicho

Ni nini kinachosababisha retinopethia ya kisukari?

Kisukari kinaweza kuharibu mishipa ya damu kwenye macho. Watu wenye kisukari mara nyingi wanakuwa na shinikizo la juu la damu. Shinikizo la juu la damu linaweza kusababisha mabadiliko kwenye mishipa ya damu kwenye macho yako kiasi cha kudhuru retina zako.

Bila matibabu, retinopethia ya kisukari inakuwa mbaya zaidi kadiri unavyoendelea kuugua ugonjwa wa kisukari. Ujauzito unaweza pia kufanya retinopethia ya kisukari kuwa mbaya zaidi.

Je, ni zipi dalili za retinopethia ya kisukari?

Unaweza kuwa na dalili mwanzoni, lakini kwa kawaida retinopethia ya kisukari inasababisha:

  • Kupoteza uwezo wa kuona taratibu, kwa uhakika

  • Sehemu ya mboni isiyoona

  • Ukungu katikati ya uoni wako

Baadaye unaweza kuwa na dalili kama vile:

  • Vieleaji (madoa meusi ambayo yanaonekana kujongea katika uoni wako)

  • Mweko wa mwanga

  • Upotevu mkubwa wa uoni wa ghafula, bila maumivu

Kutegemeana na eneo la retina ambalo limeharibiwa, baadhi ya watu hawana tatizo la kupoteza uwezo wa kuona hata kama retinopethia ya kisukari ni mbaya sana.

Madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa retinopethia ya kisukari?

Ili kujua ikiwa una ugonjwa wa retinopethia ya kisukari, madaktari watafanya haya:

  • Watatumia ofthalmoskopu (kifaa chanye mwanga kwa ajili ya kuangalia ndani ya jicho) ili kuona mishipa ya damu inayovuja na ukuaji wa mishipa mingine isiyo ya kawaida

  • Atakudunga sindano kwenye mshipa wako kuweka rangi maalumu ambayo inawasaidia madaktari waone mishipa ya damu kwenye jicho lako (mchakato unaoitwa angiografia ya fluorescein)

  • Kupiga picha ya retina yako

Je, madaktari wanatibu vipi retinopethia ya kisukari?

Kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu na shinikizo la damu ni muhimu. Madaktari watakupa dawa na kukwambia jinsi gani mlo mzuri unaweza kukusaidia kudhibiti sukari kwenye damu na shinikizo la damu. Pia ni muhimu kwamba:

  • Kupima sukari kwenye damu yako na shinikizo la damu mara kwa mara

  • Kupimwa macho yako na daktari wa macho

  • Usivute sigara, au uache ikiwa unavuta

Daktari wako pia anaweza kukupa:

  • Upasuaji mdogo ili kuzuia mishipa ya damu isivuje

  • Chanjo kwenye macho yako ili kupunguza kasi ya ukuaji wa michipa mipya ya damu isiyo ya kawaida

  • Utaratibu mwingine wa upasuaji ikiwa retinopathi inasababisha kuvuja damu sana au retina iliyobanduka