Kubanduka kwa Retina

(Retina Iliyobanduka)

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Retina ni safu ya seli nyuma ya jicho lako ambayo hutambua mwangaza na kutuma mawimbi kwenye ubongo ili kukuwezesha kuona.

Retina Iliyobanduka ni nini?

Retina iliyobanduka ni ile ambayo imejitenga na sehemu ya nyuma ya jicho. Sehemu au retina yako yote inaweza kuwa imebanduka.

  • Una uwezekano mkubwa wa kuwa na retina iliyobanduka ikiwa unaona vitu vya karibu tu (unapata shida kuona vitu vya mbali kwa udhahiri), ulifanyiwa upasuaji wa macho au ulipata jeraha la jicho

  • Dalili zinajumuisha kukosa uoni kwa ghafula au kuona mwanga mkali wa kumweka au vieleaji (madoa meusi yanayoonekana yanatembea kwenye uoni wako)

  • Inaweza kuonekana kama pazia au kitambaa kilichoshushwa kuziba uoni wako

  • Madaktari wanaweza kuona retina iliyobanduka kwa kuangalia jicho lako kwa hadubini maalumu

  • Kwa kawaida matibabu yanaweza kukusaidia usipoteze uoni

Katika hali fulani, huenda usiwe na uwezo wa kuona tena. Ikiwa una dalili zozote mwone daktari wa macho haraka ili kuzuia kupoteza kabisa uwezo wa kuona.

Kuangalia Retina

Nini kinasababisha retina iliyobanduka?

Retina inaweza kubanduka baada ya kuchanika. Kuchanika kwa retina hutokea mara nyingi zaidi unapokuwa mtu mzima na endapo una:

  • Mayopia kali (una tatizo kuona kwa udhahiri vitu vilivyo mbali)

  • Ulifanyiwa upasuaji ili kuondoa mtoto wa jicho (hali ya ukungu kwenye lenzi ya jicho lako)

  • Jeraha la jicho

  • Retina yako kusinyaa na kuwa na makovu, kwa kawaida kwenye ukingo au machozi kidogo kwenye retina

  • Kukauka na kusinyaa kwa kiowevu kinachofanana na mafuta ya mgando mbele ya retina ambacho kinaivuta kutoka nyuma ya jicho

  • Kiowevu au damu kujikusanya nyuma ya retina

  • Magonjwa mengine yanayoathiri retina, kama vile kisukari

  • Wanafamilia ambao wamewahi kuwa na retina iliyobanduka

Dalili za retina iliyobanduku ni zipi?

Watu wengine hawana dalili zozote. Ikiwa una dalili, hutahisi maumivu yoyote, lakini unaweza kwa ghafula unaweza kuwa:

  • Vieleaji vingi sana (madoa meusi ambayo kiukweli hayapo hapo lakini yanaonekana kujongea katika uoni wako)

  • Mweko wa mwanga mkali

  • Uoni hafifu

  • Kupoteza uwezo wa kuona kwenye kingo na kuenea ndani

  • Hali ya kijivu katika eneo lako la kuona ambayo inaonekana kama pazia au kitambaa kikishuka kwenye uoni wako

  • Wakati mwingine unapoteza uwezo wa kuona haraka

Kubanduka kwa retina kwa kawaida hutokea kwenye jicho moja kwa wakati.

Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina retina iliyobanduka?

Madaktari watafanya:

  • Wanaweka dawa ya matone kwenye macho yako

  • Wanaangalia retina yako kwa kutumia ofthalmoskopu

  • Wakati mwingine, wanatumia kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti ili kuona picha za nyuma ya macho yako

Je, madaktari wanatibu vipi retina iliyobanduka?

Madaktari wanatibu hali ya kubanduka kwa namna tofuati kulingana na kisababishi. Madaktari watarekebisha retina iliyobanduka au kuchanika kwa:

  • Kuingiza hewa au gesi kwenye jicho ili kurudisha retina kwenye sehemu yake

  • Kubonyeza sehemu ya nje ya jicho ambapo mbanduko upo ili kusaidia kulibandika tena

  • Wakati mwingine, kuweka mpira wa silkoni kwenye jicho lako (inaitwa bakoli ya sklera)

Ikiwa retina imechanika kwa ndani, daktari atatumia leza au kifaa cha kugandisha ili kuziba sehemu iliyochanika na kuzuia eneo hilo lisibanduke.

Kwa kawaida, uoni wako unarejea baada ya daktari kurekebisha retina yako. Huenda ukapoteza kabisa uwezo wako wa kuona ikiwa:

  • Retina yako ilibanduka kwa siku au wiki kadhaa

  • Unavuja damu au makovu kwenye jicho lako

  • Makyula yako ilibanduka au kujeruhika

Makyula ni sehemu ndogo ya retina ambayo ina kusanyiko mkubwa wa seli zinazotambua mwangaza. Makyula ni muhimu kwa kuangalia kitu kwa kina unapoangalia kitu moja kwa moja.