Kuharibika kwa Makyula kutokana na Umri (AMD au ARMD)

(Kuharibika Kwa Makyula kutokana na Uzee)

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Retina ni safu ya seli nyuma ya jicho lako ambayo hutambua mwangaza na kutuma mawimbi kwenye ubongo unaokuwezesha kuona.

Makyula ni sehemu ndogo ya retina ambayo ina kusanyiko mkubwa wa seli zinazotambua mwangaza. Makyula ni muhimu kwa kuangalia kwa kina unapoangalia kitu. Kwa mfano, makyula yako inakusaidia kusoma au kuendesha gari.

Kuharibika kwa makyula kutokana na umri ni nini?

Kuharibika kwa makyula kutokana na umri (AMD) ni ugonjwa wa macho ambao unasababisha makyula kupoteza umbo lake la kawaida (huitwa kuharibika). Pale ambapo makyula haifanyi kazi vizuri, unapoteza sehemu ya katikati ya uoni wako. Uoni wa katikati ni mabali ambapo unaona vitu vidogo kwa kina.

  • AMD inapatikana sana kwa watu wenye umri mkubwa.

  • Hali inapokuwa mbaya zaidi inaweza kusababisha upofu

  • Vitamini fulani vinaweza kusidia kupunguza upotevu wa uoni kutokana na AMD

  • Baadhi ya watu wanahitaji matibabu ili kupunguza upotevu wa uoni kutokana na AMD

Kuna aina mbili za AMD. Kwanza unapata:

  • AMD kavu, ambapo seli katika makyula zinakufa taratibu na kusababisha upotevu wa uoni wa taratibu

Baada ya kuwa umepata AMD kavu kwa muda, unaweza kupata:

  • AMD chepwe, ambapo mishipa ya damu mipya ya kawaida inakuwa chini ya makyula iliyoharibika na kuvujisha damu na kusababisha kupotea haraka uwezo wa kuona

Viewing the Retina

Ni nini kinasababisha AMD?

Madaktari hawajui kinachosababisha AMD. Hali fulani zinaongeza hatari ya kuipata. Uwezekano wako wa kupata AMD ni mkubwa ikiwa:

  • Zaidi kwa umri

  • Una wanafamilia wenye AMD

  • Uvutaji sigara

  • Una ugonjwa wa moyo

  • Kuwa na shinikizo la juu la damu

  • Una uzani mkubwa kupita kiasi

  • Una matatizo fulani ya vinasaba

Je, ni zipi dalili za AMD?

Dalili za AMD hutegemea ni aina gani ya AMD uliyo nayo.

Kwenye AMD kavu:

  • Kidogokidogo, utaona vitu vichache au kupata sehemu usizoona katikati ya uoni wako

  • Unaona mstari ulionyooka kama wenye mawimbi

  • Unakuwa na dalili zilezile kwenye macho yote mawili

  • Bado una uoni wa kutosha kuweza kusoma na kuendesha

Baadaye, baadhi ya watu wenye AMD kavu wanaweza kuwa na AMD chepwe.

Kwenye AMD chepwe, dalili za kawaida hujumuisha:

  • Kupoteza uoni kwenye jicho moja jambo linalotokea haraka, kwa kawaida kwa siku au wiki kadhaa

  • Sehemu yenye ukungu au mawimbi katika sehemu ya katikati ya uoni wako

  • Dalili katika jicho moja tu kwa wakati

  • Wakati mwingine, upofu katika jicho moja

Madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa AMD?

Uchunguzi wa jicho kwa kawaida unaonesha ikiwa una AMD. Madaktari wanaangalia kuona ikiwa una upotevu wa uoni. Watakuambia uangalie mistari kuona ikiwa unaona misitari inaonekana kuwa wima au ya mawimbi.

Madaktari wanaweza kupiga picha maalumu ya retina yako au kufanya vipimo ili kuangalia sehemu za ndani za jicho lako. Kwa kawaida wanaweza kuona uharibifu kwenye jicho lako hata kabla hujaona dalili.

Je, madaktari wanatibu vipi AMD?

Ikiwa una AMD ndogo, hutapewa matibabu. Lakini daktari anaweza kukupa vitamini zifuatazo ili kufanya AMD isiwe mbaya:

Usitumie beta-carotene au vitamini A ikiwa umewahi kuwa mvutaji wa sigara kwa miaka 7 iliyopita au zaidi kwa sababu zinaweza kuongeza uwezekano wako wa kupaa saratani ya ini.

Ikiwa una hali mbaya ya kupoteza uoni kutokana na AMD, datari wako anaweza:

  • Kukuchoma sindano nyuma ya macho yako

  • Kutumia mwangaza rasmi au lesa kutibu mishipa ya damu kwenye jicho lako

  • Kupendekeza zana zinazokusaidia kusoma, kama vile vikuza maandishi, miwani maalumu za kusomea na vifaa vingine vya kusomea

  • Kuweka darubini ndogo kwenye jicho lao, ikiwa hali yako ya uoni ni mbaya na haijaimarika kupitia matibabu mengine

Ninawezaje kuzuia AMD?

Unaweza kusaidia kuzuia au kupunguza AMD ikiwa:

  • Utaacha kuvuta sigara au usianze kuvuta sigara

  • Utakula zaidi vyakula vyenye asidi ya omega-3, kama vile aina fulani za samaki na mboga za majani za rangi ya kijani kibichi

  • Utatumia vitamini zinazotumika kutibu watu ambao tayari wana AMD

  • Utadhibiti shinikizo la damu na kudhibiti uzani wako