Pua na Sanasi

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Je, pua ni nini?

Pua ni moja kati ya ogani zako za hisia na ina kazi 2 muhimu:

  • Kupumua

  • Kunusa

Sehemu ya juu ya pua imeumbwa kwa mfupa. Sehemu ya chini ya pua imeumbwa kwa gegedu. Gegedu ni tishu nyororo, ngumu.

Ndani ya pua yako kuna nafasi iliyowazi inayoitwa njia ya puani. Imefunikwa na utando wenye mishipa mingi ya damu. Seli za utando huu hutengeneza kamasi (dutu iliyolowa yenye kunata). Pia zina nywele ndogo (vijisinga) ambavyo husaidia kuchuja uchafu kutoka kwenye hewa.

Je, sanasi ni nini?

Sanasi ni nafasi tupu zilizo nyumba na zinazozunguka pua yako. Kwa sababu sanasi zina uwazi, fuvu lako halina uzito mkubwa kama ambavyo lingekuwa nao iwapo zingekuwa mfupa mgumu.

Kama ilivyo kwa njia yako ya puani, sanasi zako zimefunikwa na utando amabo hutengeneza ute na una nywele ndogo zinazonasa vumbi.

Kila sanasi yako ina uwazi mdogo ambao unaungana na njia yako ya puani. Uwazi huu huruhusu shinikizo la hewa iliyo katika sanasi zako kuwa sawa na hewa ya nje hivyo shinikizo lisije kuongezeka na kusababisha maumivu.

Locating the Sinuses

Je, pua hufanyaje kazi?

Pale hewa inapopita katika pua yako:

  • Pua hupasha joto na kuongeza unyevunyevu kwenye hewa

  • Ute na vijisinga huchuja uchafu ili usifike kwenye mapafu yako

  • Seli pokezi zilizo juu ya njia yako ya puani hutambua harufu

Hisia ya harufu ni tata. Kuna uwezekano wa harufu nyingi, nyingi zaidi ya ladha.

Unaponusanusa kwenye hewa, hewa hupita kwenye seli pokezi chini ya njia yako ya puani. Kila seli huhisi kemikali ya tofauti. Seli zinapohisi kemikali fulani, hutuma ujumbe wa neva kwenye ubongo kupita neva za harufu. Ubongo wako hutafsiri ujumbe huu kama harufu.

Kiungo cha chakula kinajumuisha harufu na ladha. Pua zako zinapokuwa zimejaa, hewa chache inaweza kufikia seli pokezi za harufu. Hii ndio sababu, wakati una mafua, chakula kinaweza kisiwe na ladha nzuri kama kawaida.

Je, ni matatizo gani yanaweza kutokea kwenye pua na sanasi?

Matatizo ya pua na sanasi ni pamoja na: