Je, koo ni nini?

Koo lako ni sehemu ya mwili wako iliyo nyuma ya mdomo/kinywa chako chini hadi kwenye njia za kupitisha vitu zinazoelekea kwenye mapafu na tumboni mwako. Jina la kitabibu la koo ni koromeo.

Koo ni njia muhimu ya kupitisha vitu:

  • Hewa hupitia kwenye koo wakati ikielekea ndani na kutoka nje ya mapafu yako

  • Chakuka hupita kwenye koo lako wakati kikielekea kwenye tumbo lako

A Look Inside the Nose and Throat

Je, zipi ni sehemu kuu za koo?

Sehemu muhimu za koo lako ni pamoja na:

  • Findo

  • Kimeo

  • kisanduku cha sauti

  • Kimio

Findo ni viuvimbe viwili vya tishu nyuma ya kinywa chako, kimoja kila upande wa koo lako. Findo husaidia kupambana na maambukizi. Findo huwa kubwa sana kwa watoto na hupungua kwa kadiri mtoto anavyokua.

Kimeo ni kipande cha tishu ambacho kinaning'inia nyuma ya koo lako katikati ya vifundo.

Kisanduku cha sauti pia hujulikana kama zoloto. Inajumuisha nyuzi za sauti na hutengeneza sauti na maneno ya sauti yako.

Epiglotitisi ni kipande cha gegedu la mbele ya kisanduku cha sauti. Unapomeza, hufunika uwazi wa zoloto ili chakula na maji visiweze kuingia kwenye mapafu.

Je, koo hufanyaje kazi?

Koo lako lina misuli midogo mingi ambayo hufanya kazi kwa kushirikiana na ulimi wako ili kukuruhusu kumeza chakula na maji na kutoruhusu yaingie kwenye mapafu. Misuli hii na misuli mingine midogo pia husaidia kudhibiti sauti yako.

Je, ni matatizo gani yanayoweza kutokea katika koo?

Matatizo ya koo ni pamoja na:

  • Maambukizi, kama vile mafindofindo na epiglotitisi

  • Vitu kutoka nje, kama vile mfupa wa samaki, kunasa kwenye koo

  • Saratani, hasa kwa watu ambao wanatumia tumbaku