Bronkiolitisi

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Bronkiolitisi ni nini?

Bronkiolitisi ni kuvimba kwa njia ndogo za hewa kwenye mapafu kwa watoto wachanga na watoto chini ya miaka 2. Kuvimba huko hufanya iwe vigumu kwao kupumua.

  • Bronkiolitisi husababishwa na maambukizi kutoka kwenye virusi

  • Mtoto wako anaweza kuwa na makamasi kwenye pua, homa, kikohozi, kuforota, na wakati mwingine shida ya kupumua

  • Watoto wengi hupata nafuu nyumbani baada ya siku 3 hadi 5, lakini wengine huhitaji kulazwa hospitalini

  • Bronkiolitisi hutokea zaidi kwa watoto chini ya miezi 6

Ni nini husababisha bronkiolitisi?

Virusi kadhaa tofauti vinaweza kusababisha bronkiolitisi. RSV (virusi vya maradhi ya kupumua) ndiyo kisababishi kinachojulikana zaidi. Bronkiolitisi hutokea sana wakati wa baridi ambapo virusi huenea kwa urahisi.

Madaktari wanafikiri ugonjwa wa bronkiolitisi unaweza kutokea sana na mbaya zaidi kwa watoto ambao mama zao huvuta sigara, hasa ikiwa mama zao walivuta sigara wakati wa ujauzito.

Dalili za bronkiolitisi ni zipi?

Mwanzoni, mtoto wako hupata dalili za mafua, kama vile:

  • Pua zinazotoa kamasi

  • Kupiga chafya

  • Kukohoa

  • Homa kidogo (100° hadi 101° F au 37.8° hadi 38.3° C)

Kikohozi kinaweza kudumu kwa wiki 2 hadi 3 au zaidi.

Baada ya siku 3 hadi 5, mtoto wako anaweza kupata:

  • Kupumua kwa shida—mtoto anaweza kuvuta pumzi haraka na kutoa sauti ya juu anapotoa pumzi (kuforota)

Watoto wengi wenye bronkiolitisi hupata dalili ndogo tu.

Katika bronkiolitisi kali, mtoto wako anaweza kuwa na matatizo mengi ya kupumua na dalili kama vile:

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana bronkiolitisi?

Madaktari wanaweza kujua kama mtoto wako ana bronkiolitisi kulingana na dalili. Daktari anaweza pia:

  • Kupima kiwango cha oksijeni katika damu ya mtoto wako kwa kutumia kitambuzi kwenye kidole cha mtoto wako (upimaji wa oksijeni)

  • Kuchukua sampuli ya kamasi kutoka pua ili kupima virusi

  • Wakati mwingine, kufanya eksirei ya kifua

Madaktari hutibu vipi bronkiolitisi?

Madaktari watakuagiza uwatibu watoto wenye dalili zisizo kali nyumbani:

  • Kumpa kiasi kidogo cha vinywaji wazi kama vile maji au juisi mara nyingi wakati wa mchana

Ikiwa mtoto wako ana shida nyingi za kupumua, anaweza kulazwa hospitalini. Kawaida, madaktari watafanya haya:

  • Kumpa mtoto wako oksijeni kupitia maski ya uso

  • Kumpa viowevu kupitia IV (kwenye mshipa)

Antibiotiki haziponyi bronkiolitisi.