Je, kudhoofika kwa misuli ni nini?
Kudhoofika kwa misuli ni kikundi cha magonjwa ambayo hutoka kwa mzazi (kurithi) ambapo misuli hupotea.
Watu wenye hali ya kudhoofika kwa misuli walirithi jeni zisizo za kawaida ambazo hudhibiti kukua na utendaji wa misuli.
Aina tofauti za kudhoofika kwa misuli huathiri aina mbalimbali ya misuli
Misuli iliyoathirika huwa imedhoofika
Wakati mwingine msuli wa moyo au misuli inayodhibiti kupumua huwa dhaifu, jambo ambalo linaweza kuwa hatarishi.
Kudhoofika kwa misuli hakuna tiba, lakini tiba ya viungo inaweza kusaidia kupunguza dalili zake
Aina za kudhoofika kwa misuli ni pamoja na:
Udhaifu wa facioscapulohumeral: hii ni mojawapo ya aina maarufu ya udhaifu wa misuli—dalili huanza kati ya miaka 7 na 20 na hujumuisha udhaifu wa misuli ya uso na mabega
Udhaifu wa misuli wa Duchenne na udhaifu wa misuli wa Becker: hizi ni aina zinazofuata kwa umaarufu na ni mbaya zaidi—udhaifu wa misuli huanza utotoni au katika miaka ya ujana, mara nyingi huwapata wavulana
Udhaifu wa Emery-Dreifuss: aina hii huathiri sehemu ya juu ya mikono, sehemu ya chini ya miguu, na mara nyingi moyo (shida ya moyo inaweza kusababisha kifo cha ghafla)
Udhaifu wa limb-girdle: Hii huathiri misuli ya mabega na nyonga
Kuna magonjwa mengine ya misuli yanayoweza kusababisha udhaifu, yakijumuisha:
Ugonjwa wa misuli ya mifupa wa kuzaliwa nao: kikundi cha matatizo ya misuli ambayo umezaliwa nayo au ambayo hujitokeza wakati ukiwa mtoto mchanga
Kupooza kwa mara kwa mara katika familia: Ni magonjwa adimu ambayo huishi katika familia na husababisha mashambulizi ya ghafla ya udhaifu au kupooza (kushindwa kusogeza kiungo au mwili wako wote)
Magonjwa ya kuhifadhi glikojeni: Kikundi cha magonjwa adimu ambayo huishi katika familia na husababisha glikojeni (wanga itokanayo na sukari) kujikusanya kwenye misuli yako
Je, nini husababisha udhaifu wa misuli?
Udhaifu wa misuli husababishwa na jeni zisizo za kawaida ambazo hurithiwa kutoka kwa mzazi. Hizi jeni zisizo za kawaida huathiri namna misuli inavyofanya kazi.
Je, dalili za udhaifu wa misuli ni zipi?
Baadhi ya aina za udhaifu wa misuli husababisha dalili kuanzia utotoni. Aina zingine usababisha dalili ambazo huanza baadaye, katika mika ya ujana au utu uzima.
Dalili zinaweza kujumuisha:
Udhaifu wa misuli
Kupooza (kushindwa kusogeza kiungo au mwili wako wote)
Ugumu wa kuinua mikono yako
Katika watoto, kuchelewa kujifunza kutembea au ugumu wa kukimbia, kuruka, au kupanda ngazi
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa ni udhaifu wa misuli?
Madaktari hushuku uwepo wa udhaifu wa misuli kutokana na dalili zako na historia ya familia. Ili kuthibitisha, daktari atafanya:
Vipimo vya damu
Uondoaji wa kipande cha msuli kwa uchunguzi (Madaktari wataondoa kipande kidogo cha msuli ili kukichunguza kwenye hadubini)
Je, madaktari hutibu vipi udhaifu wa misuli?
Hakuna tiba. Madaktari hutibu udhaifu wa mifupa kwa kutumia:
Matibabu ya kimwili
Bandeji za kukazia kifundo cha mguu au mguu
Dawa
Wakati mwingine, watu wenye udhaifu wa misuli huhitaji kidhibiti mapigo ya moyo ili kudhibiti mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.