Disleksia

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Disleksia ni nini?

Disleksia ni aina ya tatizo la kujifunza linalosababisha kuwa na matatizo ya kusoma.

Watu wenye disleksia wanapata shida ya kuhusanisha herufi na maneno na sauti zinazoyawakilisha.

  • Watoto wenye disleksia wanaweza kuchelewa kuzungumza ukilinganisha na watoto wengine

  • Wanaweza kupata shida kuzungumza, kuunganisha sauti au kutambua sauti kwenye maneno

  • Wanaweza kufanya makosa au kuchukua muda zaidi wanapotamaka herufi, kuandika au kusoma kwa sauti

  • Kujua ikiwa mtoto wako ana disleksia, wafanyakazi wa shule watampatia mtoto wako majaribio, kama vile majaribio ya kitaaluma na ya kupima akili (IQ)

  • Disleksia haiwezi kutibiwa, lakini walimu wanaweza kumsiadia mtoto wako ajifunze kutambua maneno yaliyoandikwa

Disleksia ni tofuati na kuwa na uwezo mdogo wa akili (ulemavu wa akili) Watoto wenye ulemavu wa akili wanakuwa na matatizo na mambo mengine mengi yanayohitaji kufikiri. Watoto wenye disleksia kwa kawaida wanapata shida ya kusoma tu maneno na herufi.

Je, nini husababisha disleksia?

Madaktari hawajui kinachosababisha disleksia, lakini wanajua mara nyingi huwa ni ugonjwa wa kurithi kwenye familia.

Dalili za disleksia ni zipi?

Watoto ambao hawajaanza shule wenye disleksia wanaweza:

  • Kuanza kuzungumza baadaye ukilinganisha na watoto wengine wenye umri kama wao

  • Kupata shida ya kutamka, kuchagua na kubadilisha maneno

  • Wanapata shida kukumbuka majina ya herufi, namba, rangi na picha

Watoto ambao walioanza shule wenye disleksia wanaweza:

  • Kuunganisha sauti

  • Kutamka vizuri maneno

  • Kutambua idadi ya sauti kwenye maneno na kuziweka kwenye mpangilio sahihi

  • Kugawanya maneno katika sauti

Watoto wengi wenye disleksia wanachanganya maneno, kama vile b na d, au w na m, au n na h. Wanaweza pia kugeuza herufi za neno wanaloandika kama vile ua badala ya au. Hii si dalili ya disleksia kila wakati, kwa kuwa watoto wengi wadogo wasio na disleksia pia wanafanya makosa haya wakiwa katika shule ya awali.

Ninawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana disleksia?

Ikiwa mtoto wako hafanyi vizuri katika kujifunza maneno kufikia katikati au mwishoni mwa darasa la kwanza, walimu wanapaswa kumpa majaribio mtoto wako. Wataangalia matatizo mengine ambayo yanazuia mtoto wako asiweze kusoma, kama vile uoni hafifu au kusikia au matatizo ya kihisia. Kwa kawaida, madaktari hufanya yafuatayo:

  • Majaribio ya usemi, lugha na kusikia

  • Vipimo vya uwezo wa akili

  • Majaribio ya ujuzi wa kitaaluma

Disleksia inatibiwa vipi?

Disleksia inatibiwa kwa kutumia njia maalumu za kufundishia. Njia hizi zinamsaidia mtoto wako ajifunze kutambua maneno.

Walimu wanatumia mafunzo ya kutumia milango mingi ya fahamu (ufundishaji unaojumuisha shughuli za kuona, kusikia, kusogea na miguso) ili kuwasaidia watoto:

  • Kuhusianisha herufi za alfabegti na sauti zinazowakilishwa (fonetiki)

  • Kutamka maneno

  • Kuelewa wanachokisoma

  • Kuchakata sauti, kama vile kuunganisha sauti ili kutengeneza maneno, kutengenisha maneno katika sehemu na kutambua sauti katika maneno

Watoto wakubwa wenye disleksia wanaweza kusaidiwa na teknolojia, kama vile:

  • Kusikiliza vitabu vya sauti

  • Kutumia skrini ya kompyuta inayosoma maneno kwa sauti

  • Kuchukua maelezo kwa kutumia kifaa cha kurekodia cha kidijitali

Nchini Marekani Sheria ya Elimu ya Watu Wenye Ulemavu (IDEA) ya taifa inazitaka shule za umma kutoa elimu stahiki na ya bila malipo kwa watoto wenye disleksia. Elimu inapaswa kutolewa katika mazingira yenye sheria kali, mazingira jumuishi kadiri iwezekanavyo, yaani, mazingira ambamo mtoto ana kila fursa ya kuingiliana na wanafunzi wenzake wasio na ulemavu na ana fursa sawa ya kufikia rasilimali za jumuiya.