Muhtasari wa Idadi Ndogo ya Chembe Sahani (thrombosaitopenia)

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Je, idadi ndogo ya chembe sahani ni nini?

Chembe sahani ni seli ndogo ambazo huzunguka kwenye mtiririko wa damu yako na kuisaida damu yako kuganda. Hutengenezwa katika uboho wa mifupa yako kama ilivyo kwa seli zingine za damu. Chembe sahani pia huitwa thrombosaiti.

Kwa kawaida damu yako huwa na namba fulani ya chembe sahani katika sampuli fulani ya damu. Namba hiyo ndio idadi ya chembe sahani zako.

  • Ukiwa na idadi ndogo ya chembe sahani, unavuja damu kwa urahisi

  • Huenda ukapata madoa madogo ya zambarau kwenye ngozi yako na kutokwa damu puani na kwenye fizi

  • Idadi ndogo sana ya chembe sahani inaweza kusababisha kuvuja damu kwenye ubongo wako au kuvuja damu sana kwenye utumbo wako.

  • Vitu vingi vinaweza kusababisha idadi ndogo ya chembe sahani

  • Madaktari wanaweza kufanya vipimo wakitafuta chanzo chake

  • Madaktari hutibu chanzo cha idadi ndogo ya chembe sahani na wanaweza kukufanyia upandikizaji wa chembe sahani

Je, nini husababisha idadi ndogo ya chembe sahani?

Vitu vingi vinaweza kusababisha idadi ndogo ya chembe sahani:

Je, dalili za idadi ndogo ya chembe sahani ni zipi?

Dalili kuu ya idadi ndogo ya chembe sahani ni kutokwa na damu kupita kiasi. Unaweza kuwa na:

  • Madoa madogo mekundu kwenye ngozi au mdomoni mwako

  • Michubuko baada ya majeraha madogo sana

  • Fizi kuvuja damu

  • Hedhi nzito

Uwezekano ni kuwa, chembe sahani ikipungua, utavuja damu zaidi. Walio na vigandisha damu vichache huenda wakavuja damu nyingi kwenye matumbo yao au maisha yao yakawa hatarini kwa kuvuja damu kwenye ubongo.

Je, ninahitaji vipimo gani kwa ajili ya idadi ndogo ya chembe sahani?

Wakati mwingine tatizo lililosababisha idadi yako ndogo ya chembe sahani liko wazi, kama vile ukiwa mjamzito, ukiwa na maambukizi makali, au unatumia dawa fulani.

Iwapo madaktari hawana uhakika wa sababu inayokufanya uwe na idadi ndogo ya chembe sahani wanaweza kufanya:

  • Vipimo vya damu

  • Undoaji wa sehemu ya uboho wa mifupa kwa ajili ya uchunguzi (Kuondoa sampuli ya uboho wa mifupa kwa ajili ya kuichunguza kwenye hadubini)

Je, madaktari hutibu vipi idadi ndogo ya chembe sahani?

Jambo la msingi ni kutibu kitu chochote kilichosababisha idadi ndogo ya chembe sahani. Kwa mfano, iwapo unatumia dawa ambayo imesababisha uwe na idadi ndogo ya chembe sahani, ikiwezekana daktari wako ataacha kukupatia dawa hiyo. Kama ilisababishwa na maambukizi, daktari wako atatibu maambukizi hayo.

Mara chache, madaktari watakupatia:

  • Upandikizaji wa chembe sahani

  • Dawa za kukusaidia kuboresha kuganda kwa damu yako