Limfoma zisizo za Hodgkin

(Limfoma zisizo za Hodgkin)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Limfoma zisizo za Hodgkin ni nini?

Limfoma ni saratani inayoathiri aina ya seli nyeupe za damu iitwayo limfosaiti. Limfosaiti na seli nyingine nyeupe za damu husaidia mwili wako kupambana na magonjwa.

Limfosaiti hupitia kwenye mishipa yako ya damu na kisha kupitia mfumo wa limfu. Mfumo wako wa limfu unajumuisha nodi zako za limfu na mishipa yako ya limfu. Nodu za limfu ni viungo vidogo vyenye umbo la maharagwe vinavyopambana na magonjwa na vinapatikana kwenye shingo, kinena na kwapa.

Katika limfoma, seli za lifu hukua kukuka kwa kasi zaidi na kujilimbikiza kwenye nodi za limfu na wakati mwingine kwenye ini, wengu, na ndani ya mifupa yako (kwenye uboho).

Limfoma zisizo za Hodgkin ni kundi la aina nyingi tofauti za limfoma. Zinaweza kuhusisha aina mbalimbali za limfositi. Limfoma ya Hodgkin inahusisha aina moja maalum ya limfositi.

  • Limfoma zisizo za Hodgkin hutokea zaidi kuliko Limfoma ya Hodgkin

  • Kuvimba kwa nodi za limfu ni dalili ya Limfoma zisizo za Hodgkin—nodi zako za limfu huvimba, lakini kwa kawaida hazina uchungu.

  • Unaweza kuwa na maumivu au matatizo ya kupumua ikiwa nodi za limfu zilizovimba zinabana viungo vyako

  • Matibabu yanaweza kujumuisha tiba ya mionzi, tibakemikali, dawa zingine zinazoitwa kingamwili za kloni moja, au mchanganyiko wa matibabu haya.

Madaktari hugawanya Limfoma zisizo za Hodgkin katika aina 2 kuu:

  • Limfoma tulivu, ambayo hukua polepole

  • Limfoma kali, ambayo hukua haraka

Lymfoma tulivu ni rahisi kutibu, na unaweza kuishi nayo kwa miaka mingi. Lakini kwa kawaida haina tiba. Limfoma kali inahitaji matibabu makali lakini mara nyingi inaweza kutibiwa.

Unaweza kupata Limfoma zisizo za Hodgkin ukiwa na umri wowote.

Ni nini husababisha Limfoma zisizo za Hodgkin?

Madaktari hawajui Limfoma zisizo za Hodgkin husababishwa na nini. Aina fulani zinaweza kusababishwa na virusi.

Dalili za Limfoma zisizo za Hodgkin ni gani?

Mwanzoni:

  • Tezi limfu kwenye shingo, makwapa, au kwenye kinena chako huvimba—lakini kwa kawaida haziumi.

Baadaye unaweza kuwa na dalili zingine kama:

  • Kukohoa au matatizo ya kupumua

  • Kuvimba kwenye uso, shingo, mikono na miguu

  • Kutohisi njaa au kutapika

  • Kufunga choo (kutatizika kwenda haja kubwa)

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Kupata vidonda au kutokwa na damu kwa urahisi zaidi

Kwa watoto, dalili za kwanza zinaweza kuwa tofauti na zinaweza kujumuisha:

  • Anemia (idadi ndogo ya seli nyekundu za damu)

  • Upele

  • Udhaifu na hisia zisizo za kawaida

Madaktari wanawezaje kujua kama nina limfoma isiyo ya Hodgkin?

Madaktari watashuku uwepo wa Limfoma isiyo ya Hodgkin iwapo kuna uvimbe kwenye nodi za limfu usio na uchungu na usioisha baada ya wiki chache.

Madaktari wakishuku limfoma isiyo ya Hodgkin kutokana na dalili zako, watafanya haya:

  • Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi (kuchukua sampuli ya nodu ya limfu iliyopanuka ili kuichunguza kwenye hadubini)

Kabla ya madaktari kukutibu limfoma isiyo ya Hodgkin, wanahitaji kuona jinsi ilivyoenea. Madaktari hutumia vipimo kadhaa ili kuchunguza hinsi limfoma isiyo ya Hodgkin ilivyoenea, kama vile:

Madaktari hutibu vipi limfoma zisizo za Hodgkin?

Ikiwa una limfoma tulivu, ambayo haijaenea, huenda usihitaji matibabu kwa miaka. Vinginevyo, madaktari wataanzisha matibabu mara moja. Matibabu unayohitaji yanategemea aina ya limfoma isiyo ya Hodgkin uliyo nayo na jinsi ilivyoenea mwilini mwako.

Matibabu ya limfoma isiyo ya Hodgkin yanaweza kujumuisha:

  • Kudungiwa kingamwili za kloni moja kwenye mshipa wa damu—hizi hutumia mfumo wako wa kingamwili kupambana na saratani uliyo nayo

  • Tibakemikali

  • Tiba ya mionzi

Ukipata limfoma tena baada ya matibabu yaliyofaulu (kurudi), madaktari wanaweza kujaribu: