Hodgkin Limfoma

(Limfoma ya Hodgkin; Ugonjwa wa Hodgkin)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Limfoma ya Hodgkin ni nini?

Limfoma ni saratani inayoathiri aina ya seli nyeupe za damu iitwayo limfosaiti. Limfosaiti na seli nyingine nyeupe za damu husaidia mwili wako kupambana na magonjwa.

Limfosaiti hupitia kwenye mishipa yako ya damu na kisha kupitia mfumo wa limfu. Mfumo wako wa limfu unajumuisha nodi za limfu na mishipa ya limfu. Nodu za limfu ni viungo vidogo vyenye umbo la maharagwe vinavyopambana na magonjwa na vinapatikana kwenye shingo, kinena na kwapa.

Lymphatic System: Helping Defend Against Infection

Katika limfoma, seli za limfu hukua kwa wingi usiodhibitika. Seli hizo hujilimbikiza kwenye nodi za limfu na wakati mwingine kwenye ini, wengu, na ndani ya mifupa yako (uboho).

Limfoma ya Hodgkin ni aina ya limfoma ambayo inahusisha aina fulani ya seli za limfu. Limfoma isiyo ya Hodgkin inahusisha aina nyingine za seli za limfu.

  • Limfoma ya Hodgkin huanza kwenye nodi za limfu na kuzifanya kuwa kubwa zaidi

  • Madaktari hutibu Limfoma ya Hodgkin kwa tibakemikali na tiba ya mionzi

  • Watu wengi wanaougua Limfoma ya Hodgkin wanaweza kuponywa

Ni nini husababisha Limfoma ya Hodgkin?

Madaktari hawajui Limfoma ya Hodgkin husababishwa na nini. Sio ugonjwa ambao unaweza kuambukizwa na mtu wengine.

Dalili za Limfoma ya Hodgkin ni nini?

Dalili za Limfoma ya Hodgkin zinajumuisha?

  • Kuvimba kwa nodi za limfu kwenye shingo, makwapa, au kinena—kwa kawaida hakuna maumivu lakini mara chache zinaweza kuuma saa chache baada ya kunywa pombe.

  • Homa

  • Kutokwa jasho usiku

  • Kupungua uzani

  • Kuwasha

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

Dalili zingine zinaweza kutokea kulingana na mahali ambapo seli za saratani zinakua. Kwa mfano, nodi za limfu zilizovimba kwenye kifua zinaweza kubana njia zako za hewa na kusababisha kukohoa au matatizo ya kupumua.

Madaktari wanawezaje kujua kama nina Limfoma ya Hodgkin?

Madaktari watashuku uwepo wa Limfoma ya Hodgkin iwapo kuna uvimbe kwenye nodi za limfu usio na uchungu na usioisha baada ya wiki chache.

Ili kufanya utambuzi, madaktari watafanya:

  • Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi (kuchukua sampuli ya nodu ya limfu iliyopanuka ili kuichunguza kwenye hadubini)

Kabla ya kutibu Limfoma ya Hodgkin, madaktari watahitaji kuona jinsi ilivyoenea. Madaktari hutumia vipimo kadhaa kuangalia jinsi Limfoma ya Hodgkin ilivyoenea, kama vile:

Madaktari hutibu vipi Limfoma ya Hodgkin?

Madaktari hutibu Limfoma ya Hodgkin kwa:

Limfoma ya Hodgkin ikirudi baada ya matibabu, madaktari huitibu kwa:

Baada ya matibabu, madaktari huendelea kuchunguza matatizo kwa kufanya majaribio na vipimo vya mara kwa mara kama vile eksirei na uchanganuzi wa CT wa kifua ili kuona ikiwa saratani imerejea.