Je, lukemia ni nini?
Lukemia ni saratani ya seli nyeupe za damu. Seli nyeupe za damu zina kazi nyingi, ikiwemo kusaidia mfumo wa kingamaradhi ya mwili wako kukabiliana na maambukizi. Seli nyeupe za damu hutengenezwa kwenye uboho wako, tishu nyororo ndani ya mifupa yako.
Ukiwa na lukemia, idadi yako ya seli nyeupe za damu iko juu sana. Hata hivyo, seli nyeupe za damu zenye saratani hazifanyi kazi ipasavyo, hivyo kuna uwezekano wa kupata maambukizi. Maambukizi hayo yanaweza kuhatarisha maisha.
Pia, seli nyeupe za damu zenye saratani hujaa kwenye uboho wako hivyo huwezi kutengeneza seli za damu za kawaida kama vile:
Seli nyekundu za damu (husababisha anemia)
Seli nyeupe za damu za kawaida (huongeza hatari ya maambukizi)
Chembe sahani (huongeza hatari ya kuvuja damu)
Kuna aina nyingi tofauti za seli nyeupe za damu lakini aina 2 kuu tu za lukemia:
Lukemia ya limfu: saratani inayoathiri limfu, ambayo ni aina moja ya seli nyeupe za damu
Lukemia ya uboho: saratani inayoathiri aina nyingine zote za seli nyeupe za damu
Lukemia ya limfu na uboho inaweza kuwa kali au sugu:
Kali: saratani ya seli changa ambayo huenea haraka na inaweza kusababisha kifo ndani ya miezi 3 hadi 6 isipotibiwa
Sugu: saratani ya seli zilizokomaa inayoenea polepole
Lukemia ya myeloidi ya muda mrefu (CML) ni nini?
Lukemia ya myeloidi ya muda mrefu (CML) ni aina ya saratani inayokua polepole ya aina tofauti mbalimbali za seli nyeupe za damu. Seli za saratani hukua na kusambaa kwenye damu na sehemu nyingine za mwili wako.
CML hutokea mara nyingi kwa watu wazima kati ya umri wa miaka 40 na 60
Unaweza kuhisi uchovu na kutokuwa na hamu ya kula na kupoteza uzani
Vile saratani hio inakua, unaweza pia kusawajika na kuchibuka au kuvuja damu kwa urahisi
Madaktari hupata CML kwa vipimo vya damu na uchunguzi wa uboho
CML inatibiwa kwa dawa zinaitwa TKI (vizuizi vya tairosini kainesi)
Zaidi ya asilimia 90 ya watu waliotibiwa mapema huishi angalau miaka 5
CML ina daraja 3:
awamu sugu: miezi au miaka ya kwanza wakati saratani inakua polepole zaidi
Awamu iliyoharakishwa: saratani huanza kukua haraka zaidi, matibabu hayafanyi kazi pia na dalili hukuwa mbaya zaidi
hatua ya mlipuko: seli za saratani changa zaidi zinazoitwa mlipuko hutokea na saratani huwa mbaya zaidi, kwa matatizo kama vile maambukizi na kuvuja damu hatari
Je, ni nini husababisha CML?
CML inasababishwa na tatizo kwa mojawapo ya kromosomu yako. Kila seli ya mwili wako ina kromosomu 46. Kromosomu hizo zina DNA, ambayo hubainisha jinsi seli zako zinafanya kazi.
Katika CML, mojawapo ya kromosomu zako kujenga kitu kisicho cha kawaida. Kromosomu isiyo ya kawaida inaitwa kromosomu ya Philadelphia. Huwa inatengeneza kitu ambacho hufanya aina moja ya seli nyeupe za damu ikue visivyo kawaida na kukosa kudhibitika.
Je, dalili za CML ni zipi?
Mapema, CML inaweza kukosa kusababisha dalili. Wakati dalili zinatokea mara ya kwanza, zinaweza kujumuisha:
Kuhisi udhaifu na uchovu
Kutohisi njaa
Kupungua uzani
Homa
Kutoa jasho usiku
Kuhisi kujaa kwenye tumbo ya juu (kwa sababu ya ini na wengu mkubwa)
Baadaye, unaweza kuwa mgonjwa zaidi na kuwa na dalili kama:
Homa (kutokana na maambukizi au lukemia)
Michubuko
Kuvuja Damu
Madaktari wanawezaje kujua kama nina CML?
Ili kujua kama una CML, madaktari watafanya haya:
Fanya vipimo vya damu
Chukua sampuli ya uboho wako ili upimwe (kipimo cha uboho)
Kufanya kipimo cha molekuli ili kuangalia kromosomu ya Philadelphia
Je, madaktari wanawezaje kutibu CML?
Madaktari hutibu CML kwa:
Dawa zinaitwa TKI (vizuizi vya tairosini kainesi)
Matibabu ya kuwekewa seli mpya, ikihitajika