Kidingapopo: Kile Wasafiri Wanahitaji Kujua
Maoni19/09/24 Thomas M. Yuill, PhD, University of Wisconsin-Madison

Kwa karne zilizopita, kulikuwa na hekaya za roho za mapepo wabaya waliokuwa wakinyemelea nchi za tropiki ambazo zingesababisha magonjwa makali kwa wageni. Wasafiri wangepata homa, homa ya baridi, maumivu ya kichwa, uchovu kupita kiasi na maumivu ya mwili yenye uchungu.

Leo hii, tunajua hizi kwa kweli ni dalili za kidingapopo, kisichosababishwa na roho za mapepo wabaya wanaozunguka zunguka bali husababishwa na kung'atwa na mbu. Kidingapopo ni maambukizi ya virusi yanayoletwa na mbu ambayo yanasababisha homa, maumivu ya jumla ya mwili, na ikiwa ni kali, kuvuja damu nje na ndani (hali inayojulikana kama homa ya kuvuja damu ya kidingapopo).

Kwa watu wanaoishi au kusafiri katika maeneo ambayo kidingapopo hutokea sana, kuna mambo muhimu ya kujua ili kutambua ishara za ugonjwa na kupunguza zaidi hatari ya maambukizi. Hapa kuna mambo ya kuangalia kuhusu kile ambacho watu wanapaswa kujua kuhusu kidingapopo.

1. Si mbu wote wanabeba kidingapopo

Kwa kawaida, kidingapopo kinaenezwa kwa watu kupitia kung'atwa na mbu aina ya Aedes walioambukizwa. Kila mwaka, takriban visa 50 hadi 100 vya kidingapopo na takriban vifo 20,000 hutokea dunia kote. Hata hivyo, nchini Marekani, ni takriban visa 100 hadi 200 tu ndivyo hutokea kila mwaka, karibu vyote huletwa na wasafiri wanaorejea kutoka katika maeneo yaliyoathiriwa.

2. Kidingapopo kinaenea kuelekea katika maeneo mapya

Kidingapopo hutokea zaidi katika maeneo ya tropiki na yale ya chini ya tropiki dunia kote. Hutokea zaidi katika Asia ya Kusini Mashariki lakini pia inatokea sana katika Amerika ya Kusini na ya Kati, huku idadi ya visa vya juu zaidi ikiwa ni katika nchi ikijumuisha Brazili. Mara nyingi, visa vya kidingapopo vinavyoripotiwa nchini Marekani hutokea kwa watu ambao hivi karibuni walitembelea sehemu za dunia ambapo kidingapopo hutokea mara kwa mara.

Vilevile, mbu aina ya Aedes wanatokea katika maeneo mapya kwa sababu ya shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabianchi. Nchini Marekani, wamepatikana katika majimbo ikiwa ni pamoja na Florida, Southern California, Texas, Arizona na maeneo ya Magharibi ya Kati. Visa vichache vya maambukizi ya kidingapopo nchini vimetokea Hawaii, Florida na Texas.

3. Kidingapopo hutokea katika awamu tatu

Kidingapopo kinatofautiana kwa ukali na si kila mtu anayeambukizwa huwa mgonjwa sana. Lakini kwa wale wanaoumwa sana, kinaweza kuwa hatari sana. Kwa kawaida dalili za kidingapopo huanza kwa ghafla, zikisababisha homa, homa ya baridi, maumivu makali ya kichwa, maumivu wakati macho yanaposogezwa, uchovu kupita kiasi na maumivu makali ya jumla kwa mwili, haswa kwenye mgongo, miguu na viungo. Maumivu haya mara nyingi huwa machungu sana hadi ugonjwa ukaitwa "homa ya kuvunjika mifupa."

Kwa kawaida dalili hizi hukaa kwa siku chache, ambapo baadaye wagonjwa huanza kuhisi vyema kwa takriban saa 24. Watu wanaweza kufikiria kuwa homa imeisha, lakini baadaye homa inaweza kurejea, pamoja na athari kali zaidi, ikiwa ni pamoja na homa ya kuvuja damu ya kidingapopo, kuvuja damu na mshtuko.

4. Kidingapopo hakiambukizwi

Katika matukio mengi zaidi, watu walio na kidingapopo hawawezi kuwaambukiza wengine. Mbu anaweza kukisambaza kwa kumng'ata mtu aliye na maambukizi na kisha kumng'ata mtu mwingine. Ingawa ni nadra, mwanamke mjamzito anaweza kupitisha virusi vya kidingapopo kwa kijusi chake wakati wa ujauzito au wakati wa kujifungua. Kumekuwa na ripoti moja ya virusi vya kidingapopo kupitishwa kupitia maziwa ya matiti.

5. Kwa sasa hakuna chanjo dhidi ya visa vipya

Chanjo pekee ya kidingapopo inayopatikana kwa sasa nchini Marekani imeidhinishwa kwa watoto ambao hapo awali waliambukizwa na wanaishi katika eneo ambalo ugonjwa huo hutokea mara kwa mara. Kuna chanjo zinazoendelezwa ambazo zinaweza kutumiwa kwa watu ambao hawajawahi kupata maambukizi ya kidingapopo hapo awali na pia wale ambao wamekuwa nayo.

6. Wasafiri wanahitaji kuwa waangalifu

Mtu yeyote anayesafiri katika sehemu za dunia ambapo kidingapopo hutokea sana anapaswa kuchukua hatua za kujilinda yeye mwenyewe na wasafiri wenzake. Kabla ya ziara, tembelea kliniki ya dawa za kusafiri na uzungumze na daktari kuhusu hatari na tahadhari zinazoweza kuchukulia. Mapendekezo na ushauri wa sasa unapatikana kupitia wakala wa afya kwa umma kama Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa. Kumbuka kuwa mara nyingi data inaweza kuwa katika kiwango kilichopitwa na wakati kwa hadi wiki moja.

Wakati wa kusafiri, hatua zile zile bora kabisa za kuepuka kung'atwa na mbu aina zote zinapaswa kutumika. Valia mavazi ya rangi angavu, yenye mikono mirefu, yasiyobana, yenye kukutosha vizuri. Tumia mafuta ya kufukuza wadudu. Mafuta ya kufukuza wadudu yanazidi kuongezwa katika mafuta ya kuzuia miale ya jua. Hakikisha unakagua lebo kabla ya kutumia bidhaa yoyote kwa watoto.

Hatimaye, njia bora zaidi ya kupunguza hatari ya kidingapopo ni kupunguza idadi ya mbu ambao wanaibeba. Inaweza kuwa changamoto kuondoa maeneo yote wanapozalia, lakini pia kuna hatua bunifu zinazochukuliwa ili kupunguza idadi ya mbu, ikiwa ni pamoja na kuleta mbu waliotengenezwa kijenetiki na kupitia bakteria ambao huzuia mbu kuambukizwa na kidingapopo.

7. Wasafiri wanapaswa kuangalia uwepo wa dalili

Kwa kawaida dalili za kidingapopo huanzia takriban siku 3 hadi 15 baada ya kung'atwa na mbu aliyeambukizwa. Mara nyingi, msafiri huanza kuhisi mgonjwa mara baada ya kurejea nyumbani. Ikiwa ulisafiri na umeanza kujihisi mgonjwa, ni muhimu sana kwamba utoe maelezo ya safari yako pale unapozungumza na daktari wako.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kidingapopo, tembelea ukurasa wa Miongozo au Vidokezo vya Haraka kuhusu mada hii.

dengue