Mbabuko unaotokana na jua ni nini?

Ni nini husababisha mbabuko unaotokana na jua?

Mbabuko unaotokana na jua ni wekundu unaoumiza ngozi yako unaosababishwa na miale ya UV (mnururisho) kwenye mwanga wa jua.

Una uwezekano mkubwa wa kupata mbabuko unaotokana na jua katikati ya mchana (10 AM hadi 3 PM) wakati miale ya UV ina nguvu zaidi.

Hatari ya mbabuko unaotokana na jua ni kubwa zaidi kwa watu ambao wana ngozi nyeupe, macho ya bluu, na nywele nyeupe au nyekundu; wanaofanya kazi nje; ambao wamewahi kuwa na mbabuko unaotokana na jua hapo awali.

Kwa sababu mashine ya kufanya ngozi kuwa ya hudhurungi hutumia mwanga wa UV kukupa rangi ya hudhurungi, unaweza pia kubabuka ngozi kwa kukaa muda mrefu kwenye mashine hiyo.

Dalili za mbabuko unaotokana na jua ni gani?

Dalili zinaweza kuanza saa moja baada ya kuungua na huwa mbaya zaidi katika saa 12 hadi 24 baada ya kuungua. Utakuwa na ngozi nyekundu yenye maumivu; makovu; homa, mzizimo, na udhaifu ikiwa kuungua kwako ni kukali.

Siku chache baadaye, sehemu iliyochomeka itakuwa na mwasho kisha ngozi itatoka.

Mara nyingi ngozi iliyobabuka kutokana na jua inapata maambukizi.

Ikiwa jua lilikuchoma vibaya ulipokuwa mchanga, una hatari kubwa ya kupata melanoma (aina ya saratani ya ngozi).

Madaktari hutibu vipi mbabuko unaotokana na jua?

Kwa mbabuko mdogo unaotokana na jua, madaktari watakuambia:

  • Chukua dawa ya maumivu isiyo ya maagizo.

  • Oga kwa maji baridi ya rasharasha au beseni.

  • Weka kitambaa baridi, mafuta ya kujipaka, aloe, au losheni ya kuongeza unyevu kwenye mbabuko wako uliotokana na jua.

Ili kutibu mbabuko unaotokana na jua, madaktari wanaweza kukupa malai yenye dawa ya kuua bakteria ili upake kwenye makovu yako. Usiponde makovu yako na epuka kuweka ngozi yako iliyo na mbabuko unaotokana na jua katika mwanga wa jua kwa wiki kadhaa.

Je, ninawezaje kuzuia mbabuko unaotokana na jua?

Njia bora ya kuzuia mbabuko wa ngozi unaotokana na jua ni kutokaa juani. Kuna uwezekano mkubwa wa kupata mbabuko unaotokana na jua kati ya saa 4 asubuhi na 9 mchana; katika miinuko ya juu; na wakati jua linapoakisiwa na theluji, maji au mchanga.

Wakati unalazimika kutoka nje kwenye jua, kaa nje kwa muda usiozidi dakika 30; vaa kofia yenye bavu pana, miwani ya jua, na nguo za kinga; na tumia mafuta ya kukinga jua.

Vidokezo vya kutumia mafuta ya kujikinga jua:

  • Chagua mafuta ya jua yanayostahimili maji na yenye SPF (hoja ya kweli ya ulinzi dhidi ya jua) ya 30 au zaidi.

  • Tumia mafuta ya kukinga jua yanayolinda dhidi ya miali ya UVA na UVB.

  • Tumia kiasi cha mafuta ya kukinga jua ili kufunika mwili wako.

  • Tumia mafuta ya kukinga jua dakika 30 kabla ya kutoka nje na utumie tena kila baada ya saa 2.

Kwa maeneo madogo, fikiria kutumia kikinga jua ambacho kinazuia kimwili karibu mwanga wote kufikia ngozi yako.

Hakimiliki © 2023 Merck & Co., Inc., Rahway, NJ, USA na washirika wake. Haki zote zimehifadhiwa.