Rosasia ni Nini?
Rosasia ni ugonjwa wa ngozi ambao hufanya pua yako na eneo linaloizunguka kuwa jekundu, kuvimba, na kufunikwa na chunusi ndogo na mishipa ya damu iliyovimba. Ni kawaida kwa watu wenye umri wa miaka 30 hadi 50, hasa watu wa asili ya Ireland na Ulaya ya Kaskazini.
Je, nini husababisha rosasia?
Madaktari hawajui kinachosababisha rosasia. Walio na ngozi nyororo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu.
Dalili za rosasia ni zipi?
Rosasia hukuathiri uso na kichwani pekee. Kwa kawaida hali yake huzidi kuwa mbaya baada ya muda. Kwanza, ngozi ya mashavu yako na pua huwa nyekundu kwa kipindi kirefu kuliko kawaida na inaweza kuchoma lakini vinginevyo ni kawaida. Ikiwa rosasia itaendelea, mara nyingi ngozi yako huwa na mwonekano mwekundu na kuvimba, yenye mishipa midogo ya damu yenye kuonekana chini tu ya tabaka la juu la ngozi. Unaweza kupata vichunusi vidogo. Katika hatua za mwisho, ngozi ya uso wako huongezeka unene, hivyo kuonekana nyekundu na iliyovimba.
kinaweza kuchochea rosasia?
Vyakula vyenye viungo vingi, pombe, vinywaji vya moto, malai ya kuzuia miale ya jua, msongo wa mawazo, mwanga wa jua au upepo, mazoezi, kuoga maji ya moto, na baadhi ya dawa.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina rosasia?
Daktari anaweza kubaini ikiwa una rosasia kwa kuangalia uso na kichwa chako.
Je, madaktari hutibu vipi rosasia?
Matibabu hujumuisha kujiepusha na vichochezi; leza au elektrokodari (mkondo wa umeme kwenye ngozi yako ili kutibu mishipa ya damu inayoonekana); kusugua ngozi (hatua ya kusugua na kuondoa ngozi ya ziada); au upasuaji ili kuondoa ngozi ya ziada.
Hakimiliki © 2023 Merck & Co., Inc., Rahway, NJ, USA na washirika wake. Haki zote zimehifadhiwa.