
Kiharusi cha joto ni nini?
Kiharusi cha joto ni hali ya dharura inayosababishwa na joto la mwili kupanda sana.
Mwili wako usipopoa vya kutosha kwa haraka, kiharusi cha joto kinaweza kuharibu ogani zako, kama vile ubongo, moyo na mapafu yako Inaweza pia kusababisha kifo.
Kiharusi cha joto kinaweza kumuathiri mtu yeyote. Wale walio kwenye hatari ya juu wanajumuisha watu wazee ambao waliojifungia kwenye chumba ambacho hakina kidhibiti joto hata kama chumba hicho hakionekani kuwa na joto jingi; mtu aliyefungiwa kwenye gari yenye joto jingi, haswa watoto ambao ni wachanga sana kuweza kufungua mlango (magari yanajulikana kuongeza joto ndani kwa haraka sana, haswa kwenye jua); na wanariadha na watu wanaofanya kazi kwenye joto la juu.
Ikiwa unakuwa mgonjwa kutokana na jua, huenda usitambue kuwa halijoto ya mwili wako iko juu sana.
Huenda ukaona dalili zifuatazo kama onyo la kiharusi cha joto:
Udhaifu, kizunguzungu au wepesi wa kichwa
Maumivu ya kichwa
Kuhisi mgonjwa tumboni
Kutapika
Ikiwa ngozi yako ni moto, yenye wekundu au kavu na unaonyesha dalili za kuchanganyikiwa, hivi ni viashiria vya mshtuko wa joto. Unaweza kutokwa au kutotokwa na jasho ikiwa una kiharusi cha joto.
Kiharusi cha joto hugunduliwa kulingana na kile kilichokupata, dalili zako na halijoto ya mwili wako. Daktari wako atafanya kipimo cha damu na mkojo ili kuona kama viungo vyako vinafanya kazi vizuri.
Ili kuzuia kiharusi cha joto wakati kuna hali ya joto huko nje, ni muhimu kuvaa nguo nyepesi ambazo hazibani sana, kuepuka kukaa kwenye jua kwa kadiri uwezavyo, kunywa viowevu vya kutosha hata kama hauhisi kiu na kuepuka mazoezi makali nyakati za siku zenye joto kali.
Muulize daktari wako iwapo tatizo lolote la kiafya ulilonalo au dawa zako zinaweza kuongeza hatari yako ya kupata kiharusi cha joto
Kuangalia watu wazee, haswa wale ambao hawana vidhibiti joto na kutowahi kumwacha mtoto mchanga kwenye gari lililoegeshwa.
Ikiwa unajua kuwa utafanya kazi au mazoezi kwenye joto, fanya mwili wako uzoee joto hatua kwa hatua. Kuwa sawa kimwili ni tofauti na kuzoea joto.
Hakimiliki © 2023 Merck & Co., Inc., Rahway, NJ, USA na washirika wake. Haki zote zimehifadhiwa.