Selulitisi ni Nini?

Selulitisi ni nini?

Selulitisi ni maambukizi ya bakteria kwenye ngozi yaliyoenea sana ambayo yanaweza kusambaa haraka na yanaweza kuwa mabaya sana

Selulitisi inasababishwa na bakteria ambao wanaweza kuingia kwenye ngozi yako. Bakteria wana uwezekano wa kuingia kwenye ngozi yako pale ulipojikata, sehemu ulipoumwa na mdudu, mkwaruzo, jeraha la kuungua, jeraha la kutobolewa, au mabaka ya ngozi kavu.

Selulitisi mara nyingi unasababishwa na bakteria aina ya staphylococcus

Dalili za selulitisi zinajumuisha wekundu wa ngozi, kuvimba, joo, maumivu, na wakati mwingine malengelenge yakiwa na kiowevu cha manjano.

Pia unaweza kupata homa na vinundu vya limfu vilivyovimba.

Maambukizi haya yanatokea sana kwenye miguu yako lakini yanaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili.

Kwa siku chache, inaweza kubadilika kutoka kuwa doa na kusambaa kwenye sehemu yote ya chini ya mguu wako.

Ikiwa maambukizi yataingia kwenye mtiririko wa damu, unaweza kuwa na homa kali, shinikizo la chini la damu na baadhi ya ogani zako kuacha kufanya kazi.

Hatari ni ya juu kwa watu wenye uzani mkubwa kupita kiasi, wana mfumo wa kingamaradhi ulio dhaifu, wana magonjwa mengine ya ngozi (kama vile eksema au mguu wa mwanariadha), tayari una mkono au mguu uliovimba, unatumia dawa za IV au umewahi kuwa na selulitisi kabla.

Madaktari hutambua ugonjwa wa selulitisi kulingana na mwonekano wa ngozi yako. Hakuna vipimo vya kuthibitisha kwa usahihi kabisa.

Selulitisi inatibiwa kwa kutumia dawa za kumeza za kuua bakteria, lakini wakati mwingine, ambapo kuna maambukizi makali, dawa inaingizwa kupitia mishipa hospitalini.

Ikiwa una selulitisi kwenye mguu wako, madaktari watakuomba uunyanyue.

Ili kuzuia selulitisi, safisha vidonda vya ngozi, vifunike kwa bandeji na upake dawa ya kuua bakteria kwa ajili ya ulinzi.

Unapaswa pia kutibu maambukizi ya kuvu, kama vile fangasi wa mkuuni na matatizo mengine ya ngozi ili kusaidia mipasuko yoyote kwenye ngozi ipone.

Ikiwa una kisukari au mzunguko duni, chunguza miguu yako kila siku, tumia kilainisha ngozi na uepuke majeraha kwa kuvaa viatu vizuri.

Hakimiliki © 2023 Merck & Co., Inc., Rahway, NJ, USA na washirika wake. Haki zote zimehifadhiwa.