Je, Chunusi ni Nini?
Chunusi ni tatizo la ngozi ambapo vipele hutokea kwenye uso, kifua, mabega au mgongoni.
Je, nini husababisha chunusi?
Chunusi husababishwa na mafuta ya ngozi na seli zilizokufa kuziba foliki za nywele zako. kinyweleo cha nywele kinaweza kuvimba na kutengeneza uvimbe unaoitwa chunusi yenye uwazi. Aina fulani za bakteria huingia kwenye mashina yaliyozibwa na kusababisha uvimbe. Uvimbe hutengeneza chunusi, ambazo huitwa chunusi zilizoziba ambazo zinaweza kuwa na usaha. Sababu zingine zinazosababisha chunusi ni pamoja na kubalehe, mabadiliko ya homoni mwilini mwako kwa sababu ya ujauzito au hedhi, kutumia vipodozi au malai za ngozi ambazo huziba vinyweleo, na kuvaa nguzo za kubana ambazo hunasa jasho.
Je, dalili za chunusi ni zipi?
Dalili za chunusi zinajumuisha aina mbalimbali za uvimbe kwenye ngozi yako, kama vile chunusi zenye uwazi; chunusi zilizoziba; chunusi; uvimbe mgumu, wenye kina ambao una usaha; na uvimbe mwekundu, unaouma wenye usaha.
Je, madaktari hutibu vipi chunusi?
Daktari wako anaweza kukufanya uonane na daktari wa ngozi. Kwa chunusi zote, madaktari watakufanya uoshe ngozi yako taratibu kwa kutumia sabuni ya kawaida mara moja au mbili kwa siku, na kuepuka vipodozi vyenye hali ya grisi, na kuepuka kuminya au kuchana ngozi yako kwa sababu inaweza kusababisha makovu. Kwa kutegemea hali ya chunusi zako, madaktari wanaweza kupendekeza utaratibu maalum wa kutunza ngozi au kupendekeza uonane na mshauri ikiwa unahuzunika au kujitenga kwa sababu ya chunusi zako.
Hakimiliki © 2023 Merck & Co., Inc., Rahway, NJ, USA na washirika wake. Haki zote zimehifadhiwa.