Nyenzo za Mada
Je, chunusi ni nini?
Chunusi ni tatizo la ngozi ambapo vipele hutokea kwenye uso, kifua, mabega au mgongoni. Chunusi husababishwa na mkusanyiko wa seli zilizokufa na bakteria.
Chunusi hutokea wakati ngozi iliyokufa, bakteria, na mafuta ya ngozi kavu yanajenga na kuzuia kifuko cha nywele (kifuko kidogo katika ngozi yako ambayo nywele hukua)
Madaktari hutibu chunusi kwa malai na wakati mwingine dawa ambazo utaitumia kwa njia ya kumeza
Chunusi kali zinaweza kusababisha msongo wa kihisia—huduma nzuri ya matibabu na kuonana na mshauri kunaweza kusaidia
Je, nini husababisha chunusi?
Chunusi husababishwa na mafuta ya ngozi na seli zilizokufa kuziba foliki za nywele zako. Vinyweleo vya nywele vinaweza kuvimba na kuunda uvimbe (chunusi zenye uwazi). Aina fulani za bakteria huingia kwenye mashina yaliyozibwa na kusababisha uvimbe. Uvimbe huzalisha chunusi (chunusi zilizoziba) ambazo zinaweza kuwa na usaha.
Una uwezekano mkubwa wa kupata chunusi kama wewe ni:
Kijana aliye kwenye kipindi cha kubalehe
Chunusi zinazosababishwa na kubalehe mara nyingi hupungua wakati unapofika kipindi cha kati cha miaka 20, lakini kwa baadhi ya watu, hasa wanawake, wanaweza kuwa na chunusi hadi wakiwa na miaka 40.
Sababu nyingine za chunusi:
Mabadiliko kwenye mwili wako kwa sababu ya ujauzito au hedhi
Kutumia vipodozi au malai ya ngozi ambayo huziba vinyweleo
Kutumia baadhi ya dawa, hasa kotikosteroidi au asteroidi za kujenga misuli
Kuvaa nguo za kubana ambazo hunasa jasho
Chunusi hazisababishwi na aina yoyote ya shughuli za kujamiiana au kutoosha uso wako vya kutosha. Madaktari hawafikirii kama lishe yako inahusika sana na chunusi ulizo nazo. Hata hivyo, bidhaa za maziwa na vyakula vyenye sukari nyingi vinaweza kuwa na athari kidogo.
Je, dalili za chunusi ni zipi?
Tafuta aina mbambali ya uvimbe kwenye ngozi yako kama vile:
Chunusi zenye uwazi
Chunusi zilizoziba
Chunusi
Uvimbe mgumu, wenye kina chey usaha (vinundu)
Uvimbe uchungu, mkubwa, mwekundu uliojaa usaha (uvimbe uliojaa maji au usaha)
Photo provided by Thomas Habif, MD.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina chunusi?
Madaktari wanaweza kufahamu kuwa una chunusi kwa kutazama ngozi yako.
Je, madaktari hutibu vipi chunusi?
Daktari wako anaweza kukwambia umwone daktari wa ngozi kwa ajili ya matibabu. Kwa aina zote za chunusi, madaktari watakufanya:
Uoshe ngozi yako taratibu kwa sabauni ya kawaida mara 1 au 2 kwa siku
Kuepuka matumizi ya vipodozi vyenye hali ya grisi
kuepuka kuminya au kuchana ngozi yako kwa sababu inaweza kusababisha makovu
Pia daktari anaweza:
Kukuagiza malai ya kupaka kwenye chunusi yako
Wakati mwingine, kukuandikia dawa ya kumeza ya kuua bakteria
Wakati mwingine, kupendekeza uonane na mshauri ikiwa unahuzunika au kujitenga kwa sababu ya chunusi zako
Kwa chunusi zenye hali mbaya sana, daktari anaweza kutumia dawa nyingine kama vile:
Dawa za kuzuia mimba (kwa wanawake)
Kotikosteroidi, inayoingizwa kwenye uvimbe mkubwa wenye majimaji au majipu ili kuyasaidia kupona
Isotretinoin— lakini ni pale tu ikiwa dawa zingine za chunusi zimeshindwa kufanya kazi, kwa sababu isotretinoin inaweza kuwa na athari kubwa
Kwa sababu isotretinoin ni hatari katika ujauzito, wanawake lazima watumie aina 2 za udhibiti wa uzazi wakati wa kuitumia ili kuhakikisha kuwa hawapati ujauzito.