Je, Maambukizi ya streptococcal ni Nini?

Streptokokali, kwa urahisi huitwa strep, ni kikundi cha kawaida cha bakteria.

Aina tofauti za maambukizi husababisha magonjwa tofauti.

Mara nyingi husababisha vidonda vya koo au maambukizi ya ngozi, lakini wanaweza kuasbabisha maambukizi yenye kutishia maisha katika maeneo mengine ya mwili wako.

Bakteria wa strep wanaweza kuishi ndani na kwenye mwili wako bila kusababisha dalili zozote.

Maambukizi yanaweza kutokea kwenye koo, sikio la kati, sanasi, mapafu, ngozi au tishu zako zilizo chini ya ngozi yako, vali za moyo na damu.

Maambukizi yanaweza kusababisha tishu zilizovimba zenye kuuma na nyekundu, vidonda vyenye magamba, koo kuuma, na upele.

Je, nini husababisha maambukizi ya strep?

Bakteria wa strep anaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu mwingine kwa kuvuta ndani matone yenye maambukizi kutoka kwa chafya au kikohozi cha mtu, kugusa kidonda kilichoambukizwa, au kujifungua, ambapo inaweza kusambaa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.

Je, zipi ni dalili za maambukizi ya strep?

Kama una maambukizi ya koo, unaweza kuwa na koo lenye vidonda, mabonge yaliyovimba kwenye shingo yako, homa, na usaha kwenye findo zako.

Ikiwa una maambukizi ya ngozi, unaweza kuwa na sehemu nyekundu yenye uchungu kwenye ngozi yako au vidonda vyenye magamba ya njano.

Ikiwa una maambukizi chini ya ngozi yako, unaweza kuwa na mzizimo, homa na maumivu makali na kulainika katika sehemu hiyo ya mwili. Hali hii ni mbaya sana kwa sababu inaweza kusababisha gangrini na unaweza kupoteza kiungo au hata kufa.

Je, ni matatizo gani husababishwa na maambukizi ya strep?

Homa itokanayo na baridi yabisi husababisha upate maumivu makali ya vifundo.

Watoto wanaweza kupata mishtuko ya kusogea mikono na miguu yao ambayo hawawezi kuidhibiti.

Homa ya vipele vyekundu hukusababishia upele usoni na mwili ambao unakupa hisia ya msasa. Inapopotea, ngozi yako hubanduka, na ulimi wako hupata viuvimbe vyekundu hivyo kufanana na stroberi.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maambukizi ya strep?

Daktari atapima sampuli kutoka kwenye koo lako au tishu nyingine iliyoambukizwa.

Hakimiliki © 2023 Merck & Co., Inc., Rahway, NJ, USA na washirika wake. Haki zote zimehifadhiwa.