Shambulio la Moyo

Moyo ndio ogani kuu ya mfumo wa moyo na mishipa. Ni msuli unaopiga na kusukuma damu kwenye mwili wote kwa mfululizo. Ateri za moyo husambazia moyo wenyewe oksijeni na virutubishi muhimu inavyohitaji ili kufanya kazi inavyostahili.

Seli nyekundu za damu, seli nyeupe za damu, na chembechembe zingine hutiririka kwa urahisi kwenye moyo na sehemu zngine za mwili. Kwa mtu mwenye afya bora, kuta za ateri ni nyororo na unene wake uko sawasawa. Hata hivyo, kadiri muda unavyokwenda, kiwango kikubwa cha lehemu inayozunguka kinaweza kusababisha mafuta, yaitwayo utando, yaliyorundikana.

Kadiri utando unavyorundikana, unaweza kuwa mgumu na kufanya ateri iwe nyembamba na isipitishe damu kwa urahisi, hali iitwayo atherosklerosisi. Ikiwa atherosklerosisi itatokea kwenye ateri za moyo, hali hiyo huitwa ugonjwa wa ateri za moyo, au CAD. Mtiririko wa damu ukikatizwa vibaya, shambulio la moyo linaweza kutokea. Mayokadio infakisheni, au MI, ni jina lingine la shambulio la moyo.

Uzibaji wa ateri ya moyo ukizidi asilimia 70, hatari ya kupata shambulio la moyo huongezeka; hatari hiyo ni ya hakika wakati utando umeziba kabisa ateri ya moyo.

Njia nyingine ambayo CAD inaweza kuongeza hatari ya MI ni wakati unapata damu iliyoganda. Mara nyingi, upenyu unaweza kutokea kwenye sehemu ambapo utando umerundikana. Hali hii inapotokea, damu inaweza kuganda, au kuunda bonge, katika sehemu ya upenyu, au damu iliyoganda, iitwayo thrombus, inaweza kuwa kubwa hadi izuie kabisa mtiririko wa damu.

Kiwango cha madhara ambayo moyo unapata wakati wa MI kinategemea makali yake na mahali pa uzibaji, na kasi ya kupokea matibabu. Kwa bahati nzuri, kuna njia nyingi za kuzuia atherosklerosisi, na kupunguza hatari ya kupata shambulio la moyo.