Ugonjwa wa Refluksi Gastroesofajia
Njia ya mmeng'enyo wa chakula, au GI, inajumuisha kinywa, koo, umio, tumbo, utumbo mdogo na utumbo mpana. Njia ya mmeng'enyo wa chakula ni sehemu ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, na inahusika na kuingiza na kuondoa chakula na vioevu kwenye mwili.
Pale ambapo umio na tumbo linakutana kuna msuli uitwao sfinkta ya chini ya umio, ambayo hufunguka kuruhusu chakula kuingia tumboni na kisha kufungika kuzuia chakula na asidi ya tumbo kutoka na kurudi kwenye umio. Ikiwa kuna shinikizo kubwa tumboni, au ikiwa misuli ya sfinkta haifanyi kazi inayopaswa, basi chakula iliyopo tumboni inaweza kurudi kwenye umio, na kusababisha dalili za ugonjwa wa refluksi gastroesofajia, au GERD. Dalili hizi zinaweza kujumuisha kiungulia, maumivu ya kifua, kukohoa au kushindwa kupumua unapolala, au kuzidi kwa dalili za pumu wakati unapolala.
Mlo na mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kupunguza baadhi ya dalili zinazohusiana na GERD; hata hivyo, katika hali fulani dawa au upasuaji unaweza kuhitajika.