Kujifungua Kwa Njia ya Upasuaji
Si kila mwanamke anajifungua kwa njia ya kawaida ya uke kwa kumzaa mtoto wake. Katika mazingira mabaya ya hatari au mfadhaiko wa ujauzito au ikwa utaratibu wa mtoto kuwa kinyume (mtoto anatanguliza miguu kwanza wakati wa kuzaliwa) au ikiwa mtoto wa kwanza alizaliwa kwa njia ya upasuaji, upasuaji mwingine huenda ukahitajika.
Wakati wa upasuaji, daktari ama atafanya upasuaji wa wima kwenye ngozi iliyo juu kidogo ya nywele za sehemu ya siri au mlalo chini ya kitovu.
Mkato unapofanywa, mishipa ya damu inachomwa kwa chuma au dawa kali ili kupunguza kuvuja damu. Baada ya kukata ngozi, mafuta na misuli ya tumbo, utando unaofunika viungo vya ndani unafunguliwa, ukiacha wazi kibofu cha mkojo na uterasi. Wakati huu, daktari ataingiza mikono yake kwenye pelvis ili kujua mkao wa mtoto na kondo la nyuma. Kisha, mchano unafanywa kwenye uterasi, kwa kawaida kwenye sehemu ya chini, na majimaji yoyote yanayobaki yananyonywa kutoka kenye uterasi.
Kisha daktari anapanua mchano kwa kutumia vidole vyake. Kisha kichwa cha mtoto kinakamatwa na kuvutwa taratibu pamoja na mwili wake wote kutoka kwenye uterasi ya mama.
Hatimaye, utando wa tumbo unashonwa pamoja kwa utaratibu wa kurudi nyuma tofauti na ulivyokatwa.
Mama ataachwa apone kwa takribani siku 3 hadi 5 akiwa hospitalini. Atakuwa pia na maumivu na kuzuiliwa asifanye shughuli zozote kwa wiki kadhaa zinazofuata.
Kuna matatizo kadhaa yanayohusiana na utaratibu huu ambayo yanapaswa kujadiliwa na daktari kabla ya upasuaji.