Anatomia ya Mgongo

Mgongo ni safu ya mifupa ambayo huunda mifupa ya mhimili. Mfumo huu hutoa usaidizi wenye nguvu, lakini unaonyumbulika kwa shina la mwili pamoja na ulinzi kwa uti wa mgongo uliyo ndani yake. Mgongo una pingili 33 zilizopangwa wimba kila moja juu ya nyingine. Pingili zimeunganishwa kwa viungo vya sehemu nyuma ya mgongo. Viungo hivi hurusu mifupa ya uti wa mgongo kusogea. Pingili za uti wa mgongo huwekwa katika hali ya usawa kwa kano na, muhimu zaidi, zimetenganishwa kwa kisahani cha ndani ya pingili kilicho katikati ya kila pingili, ambacho hufanya kazi kama kifyonza mshtuko. Pingili ya uti wa mgongo inaweza kugawanywa katika sehemu tano. Sehemu hizi zinajumuisha pingili 7 za shingoni, pingili 12 za sehemu ya juu na kati ya mgongo, pingili 5 za kiunoni, pingili 5 za sakramu zilizounganishwa, na pingili 4 za kitokono zilizounganishwa. Uti wa mgongo unapita katika mfereji ambao uko nyuma ya pingili, na huanzia kwenye shina la ubongo hadi kwenye eneo la kiunoni la mgongo. Neva husambaa kutoka kwenye uti wa mgongo, zikituma ujumbe wa kusogea na utendaji wa mwili kwa mwili wote. Umbo la anatomia la uti wa mgongo wa mtu mzima pia hujumuisha mipindiko minne ya msingi. Sehemu za juu na kati za mgongo na sakramu zimebonyea kwa mbele, wakati sehemu za shingoni na kiunoni zimebonyea kwa nyuma. Umbo la kipekee la uti wa mgongo huuruhusu kuhimili uzani wa mwili wa binadamu.