Mishipa ya damu: Kuzungusha Damu

Mishipa ya damu: Kuzungusha Damu

Damu husafiri kutoka kwenye moyo kwenye ateri, ambazo hugawanyika katika mishipa midogo midogo, mwishowe kuwa matawi ya ateri. Matawi ya ateri huungana na mishipa ya damu ambayo ni midogo zaidi inayoitwa kapilari. Kupitia kuta nyembamba za kapilari, oksijeni na virutibishi hupita kutoka kwenye damu na kuingia katika tishu, na takataka hutoka kwenye tishu na kuingia kwenye damu. Kutoka kwenye kapilari, damu hupita kwenye mishipa midogo/venali, kisha huingia kweye vena ili kurejea kwenye moyo.

Ateri na matawi ya ateri huwa na kuta za misuli nene kiasi kwa sababu shinikizo la damu ndani yake ni la juu na kwa sababu zinapaswa kurekebisha kipenyo chake ili kudumisha shinikizo la damu na kudhibiti mtiririko wa damu. Vena na mishipa midogo/venali zina kuta za misuli ambazo ni nyembamba na si nene sana kuliko ateri na matawi ya ateri, na sababu kubwa ni kwamba shinikizo lililo kwenye vena na mishipa midogo/venali ni la chini sana. Vena zinaweza kutanuka ili kuhimili uongezeko la ujazo wa damu.