Ili kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, Miongozo ya MSD itaangazia matukio chanya kutoka kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Hadithi za #MyPositiveMoment zitaangazia tukio la kutia moyo ambapo watu walio na virusi vya ukimwi waligundua kuwa wanaweza kuishi maisha yenye furaha na afya njema. Kutokana na hilo, tunatumai kukabiliana na unyanyapaa unaohusiana na maradhi hayo kwa kuonyesha kuwa kwa taarifa, elimu, na usaidizi unaofaa, watu bado wanaweza kusitawi.
Kupokea habari kwamba umepatikana kuwa na virusi vya ukimwi kunaweza kuwa jambo la kutisha na kuhuzunisha mno. #MyPositiveMoment inasimulia hadithi za watu watatu ambao waligundua kuwa virusi vya ukimwi havifai kuwa sifa inayoamua mwelekeo wa maisha yao. Sikiliza hadithi zao hapa:
Jennifer Vaughan
Instagram: vongirl24
Facebook: Jennifer Vaughn
YouTube: Maisha ya Chanya ya Jennifer Huku Akiishi na Virusi vya Ukimwi
Maoni ya Mtaalamu
Hivi karibuni tuliketi na mmoja wa wataalamu wetu kujadili kwa nini ni muhimu 'Kujua Hali Yako.'
Soma Maswali yetu na Majibu ya Dkt. Edward R. Cachay, Mtaalamu wa Magonjwa Yanayoambukizika, Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha California San Diego.
Tazama na Upate Ukweli wa Haraka kuhusu Virusi vya Ukimwi
Nyenzo katika Mwongozo
Taarifa za kina kuhusu virusi vya ukimwi na ukimwi
Maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa watoto
Ungana Nasi