Afya ya Pamoja

Afya ya Pamoja ni mbinu shirikishi, ya sekta nyingi, na nyanja nyingi—inayofanya kazi katika ngazi za mtaa, eneo, kitaifa na kimataifa—kwa lengo la kupata matokeo bora zaidi ya afya inayotambua uhusiano kati ya watu, wanyama, mimea na mazingira yao ya pamoja.
- Kama inavyofafanuliwa na CDC
Pitia Maswali na Majibu yetu, yaliyoandikwa kwa pamoja na mmoja wa wahariri wetu madaktari, Ernest Yeh, MD, na mhariri wa Mwongozo wa Tiba ya Mifugo, Nicholas Roman, DVM, MPH.
"Afya ya Pamoja ni wazo kwamba afya ya wanadamu, wanyama wengine na mazingira inahusiana pakubwa. Kwa hivyo, wataalamu wa matibabu na tiba ya mifugo pamoja na wale wa nyanja nyingine za sayansi, afya na mazingira wanapaswa kuwasiliana na kushirikiana, badala ya kufanya kazi peke yao."
- Nick Roman,
DVM, MPH, Mhariri wa Mwongozo wa Tiba ya Mifugo wa MSD
"Mwingiliano wa wanadamu na wanyama unaweza kukuza afya kwa njia nyingi. Watu wengi huwaona wanyama wao vipenzi kama wanafamilia, ambayo inaweza kuchangia pakubwa katika kukuza afya ya akili."
- Ernest Yeh,
Mhariri Daktari wa Miongozo ya MSD
Maudhui Yanayohusiana
Wajibu wa Tabibu wa Mifugo katika Afya ya Umma, Afya ya Pamoja
Muhtasari wa Uhusiano wa Wanadamu na Wanyama
Huduma za Familia za Tiba ya Mifugo au Huduma Zinazolingana na Uhusiano
Nyenzo za Ziada
Mwungano wa Matabibu wa Mifugo wa Marekani
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa