Siku ya Afya ya Akili Duniani


Siku hii ya Afya ya Akili Duniani, Miongozo ya MSD inachunguza uwezo wa muziki kama zana ya kujieleza na uponyaji kwa watu wanaokabiliwa na changamoto za afya ya akili zinazochochewa au kuzidishwa na athari za janga la COVID-19.

 


Muziki ni zana yenye nguvu ambayo imethibitishwa kuwa na uwezo wa kuathiri vyema afya ya akili ya watu.

#KeepMusicInMind inasimulia hadithi za wanamuziki watatu na jinsi muziki ulivyowasaidia wakati wa janga, kwa kuwasaidia kudhibiti afya yao ya akili na kuwatia moyo wengine kufanya vivyo hivyo katika kipindi kigumu cha kipekee kwa watu duniani kote.





Washa Muziki katika Nyakati Ngumu


 

Muziki kwa afya yako ya akili! Sikiliza nyimbo anazozipenda zaidi Mchangiaji wetu Mwanafunzi ambazo husaidia kuchangamsha hisia zake.

  • Get Outta My Way wa Kylie Minogue
  • Ain’t Been Done wa Jessie J
  • Higher Love wa Kygo na Whitney Houston
  • What A Wonderful World wa Louis Armstrong
  • Nothing from Nothing wa Billy Preston
  • Can’t Stop the Feeling wa Justin Timberlake
  • Study Maybe wa UMDSOM2015
  • Dynamite wa BTS
  • Some Nights wa Fun
  • I Am Here wa P!nk
  • Dancing Queen wa ABBA
  • Shut Up and Dance wa Walk the Moon

 


Sikiliza hadithi zetu


Amy Gerhartz



Amy Gerhartz ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo, mzungumzaji, kocha na mtetezi wa kujipenda. Muziki wake ni kielelezo shupavu cha jinsi safari kuelekea kuwa na afya bora ya akili huanza kwa kujali hisia zetu na mambo tunayopitia wenyewe.

Instagram: amygerhartz

YouTube: AmyGerhartz

Spotify: Amy Gerhartz

 

Samantics



Samantics ni mtunzi wa nyimbo na mshairi wa maneno ya kukariri ambaye huandika kuhusu na kupigania uelewa wa afya ya akili. Wimbo wake 'Keep Music In Mind' - ulioandikwa hasa kwa ajili ya kampeni hii - unasimulia hadithi ya safari yake ya afya ya akili katika kipindi kizima cha janga hili na jinsi alivyohisi kuwa muziki ndio aina ya usaidizi anayoipenda zaidi.

Facebook: samanticsuk

Instagram: samanticsuk

YouTube: Samantics

 

David Baquero



Wakati watu katika mtaa wake walikuwa wamentengana na kutojumuika wakati wa marufuku ya kutoka nyumbani, mwanamuziki chipukizi David alianza kuwachangamsha majirani zake kwa kucheza muziki katika roshani yake na kuunganisha eneo hilo katika sherehe isiyotarajiwa ya jamii.

Instagram: pd.baquero

YouTube: David Baquero Oficial