Kupasuka kwa Kabla ya Kujifungua kwa Utando (PROM)

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Kupasuka kwa Kabla ya Kujifungua kwa Utando (PROM)

Unapokuwa mjamzito, mtoto wako anakuwa kwenye maji ya amnioti ndani ya uterasi yako (mfuko wa uzazi). Kiowevu na mtoto anakuwa ndani ya kifuko kinachoitwa mfuko wa amnioti. Mfuko huu umeundwa na utando mwembamba lakini imara unaozuia majimaji yasivuje. Unapopata uchungu wa uzazi, mfuko wa amnioti unafunguka (unapasuka) na maji ya amnioti yanavuja kutoka kwenye uke wako. Hii kwa kawaida hurejelewa kama kupasuka kwa chupa ya uzazi. Ikiwa maji ya amnioti yanavuja kabla ya kupata uchungu wa uzazi, unapata kile kinachoitwa kupasuka mapema kwa utando (PROM).

  • Uchungu wa uzazi kwa kawaida huanza baada chupa ya maji kupasuka

  • Ikiwa uchungu wa uzazi hautaanza ndani ya saa 12 baada ya chupa ya maji kupasuka, wewe na mtoto wako mko katika hatari ya juu ya kupata maambukizi

  • Madaktari kwa kawaida wataanzisha uchungu wa uzazi kwa kutumia dawa ikiwa una wiki 34 au zaidi za ujauzito

  • Madaktari huenda wakajaribu kuondoa uchungu wa uzazi kwa kutumia dawa ikiwa ujauzito wako una chini ya wiki 34

Mpigie simu daktari wako au mkunga mara moja ikiwa unadhani chupa ya uzazi imepasuka.

Je, nitajuaje ikiwa chupa yangu ya uzazi imepasuka?

Majimaji meupe yatavuja kutoka kwenye uke wako, ama kwa kumwagika au kuchuruzika.

Baada ya chupa yako ya uzazi kupasuka, kwa kawaida utaanza kupata uchungu za uzazi ndani ya saa 12 hadi 48 ikwia una ujauzito wa zaidi ya wiki 34. Ikiwa ni rahisi kwenye ujauzito wako, inaweza kuchukua siku 4 au zaidi ili uchungu wako uanze.

Je, hatari za kupasuka kwa chupa ya uzazi mapema zaidi ni nini?

Ikiwa maji yako yatapasuka mapema sana, vijidudu vinaweza kuingia kwenye uterasi yako na kusababisha maambukizi. Unaweza kuwa na:

  • Maambukizi kwenye uterasi yako

  • Maambukizi kwa mtoto wako aliyeko tumboni

  • Mtoto wako yupo katika mkao usio wa kawaida

Maambukizi kwenye uterasi yako yanaweza kusababisha dalili kama vile:

  • Homa

  • Majimaji mazito yenye harufu mbaya kutoka kwenye uke (kiowevu)

  • Maumivu ya tumbo

Matatizo mengine unayoweza kuwa nayo ikiwa chupa ya uzazi itapasuka mapema sana hujumuisha:

  • Kondo lako la nyuma (ogani inayompa oksijeni na virutubishi mtoto aliye tumboni) ikivutika kutoka kwenye uterasi yako mapema sana (mgawanyiko wa kondo la nyuma)

  • Mtoto wako kuzaliwa mapema sana (kuzaliwa kabla ya wakati)

Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto wako uwezekano mkubwa wa:

Je, daktari wangu au mkunga atathibitishaje kwamba chupa yangu ya uzazi imepasuka?

Dakatari au mkunga atachunguza uke au mlango wa kizazi (sehemu ya chini ya uterasi yako) ili kuthibitisha kuwa chupa yako ya maji ilipasuka. Daktari au mkunga pia atakadiria ni kiasi gani cha mlango wa kizazi kimefunguka (kupanuka).

Ikiwa kuna dalili za maambukizi, daktari anaweza kuchukua sampuli ya maji ya amnioti ili kupima.

Daktari wangu au mkunga atafanya nini ikiwa chupa yangu ya maji ya uzazi imepasuka mapema sana?

Ikiwa ujauzito wako una wiki 34 au zaidi, madaktari wataanzisha uchungu wa uzazi kwa kutumia dawa (kuanzisha uchungu wa uzazi).

Ikiwa ujauzito una chini ya wiki 34, madaktari watajaribu kuzuia uchungu wa uzazi kwa kutumia dawa na kuangalia ikiwa kuna matatizo. Kawaida daktari atafanya yafuatayo:

  • Watakuweka hospitalini

  • Kukupumzisha

  • Kukupima joto lako la mwili na mapigo ya moyo angalau mara 3 kwa siku

  • Kukupa dawa za kuua bakteria ili kuzuia maambukizi

  • Kukupa dawa ili kusaidia mapafu ya mtoto aliye tumboni yakue

  • Kukupa dawa ili kuzuia ubongo wa mtoto aliye tumboni usivuje damu (ikiwa ni ujauzito wa chini ya wiki 32)

Ikiwa mtoto wako yupo kwenye shida kubwa au uterasi yako ina maambukizi, daktari wako au mkunga ataanzisha uchungu wa uzazi na kumzalisha mtoto bila kujali ujauzito wako una wiki ngapi.