Nywele za ndevu zilizozama ni nini?
Nywele za ndevu zilizozama ni chunusi ndogo, zenye uchungu kidogo kutoka kwa nywele zilizonyolewa hivi majuzi ambazo hupinda na kukua tena kwenye ngozi yako. Hii hutokea mara nyingi kwa wanaume weusi wenye nywele zenye kusokota sana. Wanawake wanaonyoa eneo lao la bikini wanaweza kupata chunusi za aina sawa kutoka kwa nywele zilizozama.
Image provided by Thomas Habif, MD.
Nini husababisha nywele za ndevu zilizozama?
Nywele za ndevu zilizozama husababishwa na nywele fupi, zenye ncha kali kurudi nyuma na kutoboa ngozi yako. Ngozi yako huwashwa na kupata uvimbe unaofanana na chunusi.
Madaktari hutibu vipi nywele za ndevu zilizozama?
Matibabu yanajumuisha:
Kukuambia uache kunyoa kwa muda
Kuwekelea kitambaa chenye joto kwenye nywele zilizozama
Kutoa nywele zilizozama na sindano safi au kichokonoo
Kuapaka dawa za kotikosteroidi au dawa za kuua bakteria
Kutumia dawa za kuua bakteria au kotikosteroidi, ikiwa una uvimbe mkali, uwekundu, na maumivu
Je, ninawezaje kuzuia nywele za ndevu zilizozama?
Njia moja ya kuzuia nywele zilizozama ni kwa kutonyoa na kuacha ndevu zako zikue, au kwa kuondoa ndevu zako kwa:
Kioevu au krimu ya kuondoa nywele
Elektrolisisi, ambayo inajumuisha kuharibu mizizi ya nywele kwa kutumia mkondo wa umeme
Matibabu ya leza
Ikiwa unanyoa, tumia njia sahihi za kunyoa:
Lowesha ndevu zako kwanza
Nyoa kwa mwelekeo ambao nywele hukua
Epuka kutumia misuguo mingi ili kupata kunyoa karibu sana