Kusokotwa kwa Korodani

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Korodani ni jozi ya viungo vya umbo la mviringo ambavyo hukaa kwenye vifuko chini ya uume. Korodani zinatengeneza manii. Manii yanatunzwe kwenye epididimisi, ambayo ni neli iliyojikuna juu ya kila korodani. Epididimisi imeunganishwe kwenye kamba ya manii. Kamba ya manii inabeba manii kutoka kwenye epididimisi kwenda kwenye mwili na inajumuisha mishipa mingi ya damua na neva.

Kusokotwa kwa korodani ni nini?

Kusokotwa kwa korodani ni pale ambapo kamba ya manii juu ya korodani inajifunga, na kukata mtririko wa damu kwenye korodani yako.

  • Ugonjwa wa kusokotwa kwa korodani unaweza kutokea katika umri wowote, lakini mara nyingi sana unatokea kwa wavulana wenye umri wa miaka 12 hadi 18 au watoto wachanga

  • Bila usambazaji wa damu, tishu za korodani zake zinaweza kufa ndani ya saa chache

Onana na daktari mara moja ikiwa unahisi una ugonjwa wa kusokotwa kwa korodani. Ni dharura ya matibabu.

Viungo vya uzazi vya mwanaume

Kusokotwa kwa Korodani ni Nini?

Nini kinababisha kusokotwa kwa korodani?

Madaktari hawajui kila wakati kinachosababisha kusokotwa kwa korodani. Baadhi ya wanaume wana ugonjwa wa kurithi ambapo kamba ya manii inakuwa kwa hali isiyo ya kawaida. Inaweza pia kutokea baada ya jeraha kwenye kinena, wakati wa kulala au kuwa nje wakati wa baridi.

Je, dalili za kusokotwa kwa korodani ni zipi?

Kusokotwa kwa korodani kunasababisha:

  • Maumivu makali kwenye korodani moja na wakai mwingine katika eneo la tumbo

  • Uvimbe wa ghafula kwenye korodani

  • Kujihisi kichefuchefu na kutapika

  • Homa

  • Haja ya kukojoa mara kwa mara

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa kusokotwa kwa korodani?

Madaktari wanashuku kuwa una ugonjwa wa kusokotwa kwa korodani kulingana na dalili ulizo nazo na kufanya uchunguzi wa kimwili. Madaktari kuthibitisha utambuzi wa ugonjwa, watafanya:

  • Kupiga picha kwa kutumia mawimbi ya sauti ili kuona mtiririko wa damu uliokatwa

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa kusokotwa kwa korodani?

Madaktari wanaweza kujaribu kurekebisha korodani kwa kufungua kwa mkono. Ikiwa hatua hiyo itafanikiwa, daktari wako atafanya upasuaji baadaye ili tezi zisijifunge tena. Ikiwa haitafanya kazi, daktari wako atafanya upasuaji mara moja ili kurekebisha korodani. Wakati wa upasuaji, daktari wako atashona tezi zote mbili ili zisijifunge tena.