Epididimitisi na Epididymo-orchitis

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Korodani ni jozi ya viungo vinavyokaa kwenye kifuko chini ya uume. Epididimisi ni neli iliyojikunja juu ya kila korodani ambapo mbegu za kiume zinahamishwa kutoka kwenye korodani na kuhifadhiwa.

Epididimitisi na Epididymo-orchitis ni nini?

Epididimitisi ni uvimbe wenye maumivu wa epididimisi.

Epididymo-orchitis ni uvimbe wenye maumivu wa epididimisi pamoja na korodani.

  • Epididimitisi na epididymo-orchitis kwa kawaida huanza kutokana na maambukizi ya bakteria

  • Madaktari hutibu magonjwa haya kwa dawa za kuua bakteria

Male Reproductive Organs

Ni nini kinachosababisha epididimitisi na epididymo-orchitis?

Epididimitisi na epididymo-orchitis kwa kawaida husababishwa na maambukizi ya bakteria. Maambukizi haya yanaweza kusababishwa na:

Wakati mwingine unaweza kupata epididimitisi au epididymo-orchitis bila kuwa na maambukizi. Madaktari wanadhani hali hii inaweza kusababishwa na kiasi cha mkojo kurudi nyuma na kusabisha mwasho.

Dalili za epididimitisi na epididymo-orchitis ni zipi?

Dalili za epididimitisi na epididymo-orchitis ni:

  • Kuvimba na ulaini karibu na korodani moja wapo

  • Maumivu ambayo yanaweza kuwa ya kudumu na makali

  • Wakati mwingine kujihisi kichefuchefu na kutapika

  • Wakati mwingine, homa

Maumivu kutokana na epididimitisi kwa kawaida yanakuja taratibu. Maumivu kutokana na epididymo-orchitis kwa kawaida yanakuja haraka sana.

Ikiwa una maambukizi ya zinaa (STI), unaweza pia kuwa na dalili zingine kama vile kutokwa vitu (majimaji angavu, ya njano au ya kijani yakitoka kwenye uume wako).

Epididimitisi na epididymo-orchitis kwa kawaida hupona haraka kwa kutibu. Lakini wakati mwingine uvimbe unaweza kutokea tena au kudumu kwa wiki kadhaa (epididimitisi sugu).

Madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa epididimitisi au epididymo-orchitis?

Madaktari wanashuku kuwa ni epididimitisi au epididymo-orchitis kulingana na uchunguzi wa kimwili. Kwa kawaida watafanya pia:

  • Kipimo cha mkojo ili kuona kama kuna maambukizi

  • Wakati mwingine, kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti, ili kuwa na uhakika kwamba huna korodani zilizosokotana (kusokotwa kwa korodani)

Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa epididimitisi au epididymo-orchitis?

Daktari atakuelekeza:

  • Tumia dawa za kuua bakteria

  • Meza dawa ya maumivu

  • Pumzika vya kutosha kadiri inavyohitajika

  • Tumia pakiti za barafu kwenye eneo lenye maumivu

  • Vaa vazi la mwanamichezo la kusaidia kukinga korodani zako (mhimili wa mwanamichezo)

Ikiwa maambukizi yatakuwa mabaya na una jipu (mkusanyiko wa usaha), daktari wako atafanya upasuaji ili kutoa usaha huo.