Majeraha ya Mgongo na Uti wa Mgongo

Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023

Je, mgongo na uti wa mgongo ni nini?

Uti wako ndio mgongo wako. Ni safu ndefu ya mifupa 24 inayoitwa vatebrae pamoja na mfupa wa kikia (sakramu). Pingili huanzia chini ya fuvu lako kwenye shingo lako na kuteremka hadi chini ya fupanyonga. Pingili za mgongo hubeba sehemu kubwa ya uzani wa mwili wako.

Kila mfupa una tundu. Matundu hayo hujipanga kutengeneza mrija unaoitwa njia ya uti wa mgongo ambao urefu wake unalingana na uti wa mgongo wako. Uti wa mgongo upo ndani ya njia ya uti wa mgongo.

Uti wa mgongo wako ni fungu la neva mfano wa waya wa umeme ambazo hupeleka na kurudisha ujumbe baina ya ubongo na sehemu zingine za mwili wako. Uti wa mgongo ni dhaifu sana, ndiyo sababu umelindwa kwenye safu ya mgongo.

  • Ishara kutoka kwenye ubongo huambia mwili wako nini cha kufanya, kama vile kusogeza mikono au miguu yako.

  • Ishara zinazoelekea kwenye ubongo hubeba taarifa kutoka kwenye mwili wako kama vile ni nini umeshika au ni wapi panapouma

  • Majeraha mengi ya mgongo na uti wa mgongo husababishwa na vitu kama ajali za magari, kuanguka, na kushiriki michezo

  • Jeraha kwenye eneo la mgongo linaweza kuathiri mifupa, neva, au uti wa mgongo

  • Majeraha ya mgongo yanauma sana

  • Majeraha ya uti wa mgongo yanaweza kukufanya uwe dhaifu au upooze, kushusha uwezo wako wa kihisia (kuhisi), na kusababisha matatizo ya kufanya ngono, kukojoa, na kujisaidia

  • Majeraha ya mgongo na uti wa mgongo wakati mwingine yanahitaji kufanyiwa upasuaji na tiba ya kimwili

Ikiwa unahisi kuwa umejeruhi mgongo au uti wa mgongo wako, mwone daktari mara moja.

Jinsi Uti wa Mgongo Ulivyo

Safu ya mifupa inayoitwa vatebrae huunda mgongo (safu ya mgongo). Vatebrae hulinda uti wa mgongo, safu ndefu, dhaifu kwenye njia ya uti wa mgongo, unaopitia katikati ya vifupa vya mgongo. Kati ya vatebrae kuna diski zinazoundwa na ufupa mwororo, ambayo husaidia kunyoosha mgongo na kukuwezesha kupinda.

Neva za uti wa mgongo: Zipo jozi 31 za neva za uti wa mgongo zinazounganika katikati. Kila neva hujitokeza kama vifupa viwili vifupi (shina).

Mashina ya usogezaji hupeleka amri kutoka kwenye ubongo na uti wa mgongo hadi sehemu nyingine za mwili, hasa kwa misuli ya mifupa.

Mashin ya hisia hupeleka ujumbe kwenye ubongo kutoka sehemu nyingine za mwili.

Kauda ekwina: Uti wa mgongo huishia karibu robo tatu ya safu ya uti wa mgongo, lakini zipo neva zinazoendelea kwenda chini. Neva hizi zinaitwa Kauda ekwina kwa kuwa inafanana na mkia wa farasi. Kauda ekwina hubeba mawimbi ya neva kwenda na kutoka kwenye miguu.

Je, nini husababisha majeraha ya mgongo na uti wa mgongo?

Majeraha ya mgongo na uti wa mgongo husababishwa na:

  • Ajali za gari

  • Kuanguka

  • Ajali za michezoni

  • Vurugu (kama vile risasi)

Je, dalili za majeraha ya mgongo na uti wa mgongo ni zipi?

Dalili za majeraha kwenye mgongo na uti wa mgongo hutegemea mahali ambapo jeraha lilipo na uharibifu wake ni mkubwa kiasi gani. Dalili zinajumuisha:

  • Maumivu kweney shingo au mgongo wako

  • Udhaifu au kiharusi (kushindwa kusogeza kiungo cha mwili wako)

  • Kupoteza uwezo wa kuhisi (ganzi)

  • Shida ya kudhibiti ni wakati gani ukojoe au kujisaidia

Sehemu za mwili wako ambazo zimeathirika hutegemea mahali ambapo uti wa mgongo umejeruhiwa. Kwa mfano, uti wa mgongo ukiharibika upande wa chini, huenda usiweze kusogeza au kuhisi chochote kwenye miguu yako lakini bado unaweza kutumia mikono yako. Lakini uti wa mgongo ukiharibiwa kwenye shingo, mikono na miguu yako yote huenda ikaathirika. Ikiwa uti wa mgongo umeharibika juu kwenye shingo yako, huenda usiweze kupumua bila usaidizi.

Udhaifu na ganzi uliyo nayo inaweza kudumu kwa muda mfupi au moja kwa moja.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina majeraha kwenye mgongo na uti wa mgongo wangu?

Madaktari watakuuliza kuhusu dalili zako na kukupima. Atafanya vipimo, kama vile:

  • Eksirei

  • Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)

  • MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku)

Je, madaktari hitibu vipi majeraha ya mgongo na uti wa mgongo?

Usimsogeze mtu mwenye majeraha ya uti wa mgongo wewe mwenyewe—subiri hadi watoa huduma ya dharura wawasili.

Watoa huduma ya dharura huzuia kusogea kwa shingo ya mtu aliyejeruhiwa (huizuia isisogee) ili kuepusha uharibifu zaidi kwa uti wa mgongo na pingili za uti wa mgongo. Huenda daktari akafanya yafuatayo:

  • Mfunge mtu kwenye ubao thabiti, ambao ni nyororo

  • Weka shingo ya mtu huyo katika kola ngumu

Pia madaktari wanaweza kutibu majeraha ya uti wa mgongo na pingili za mgongo kwa kutumia: