Wanyama wengi waouma watu nchini Marekani ni mbwa na paka:
Kuumwa na mbwa kwa kawaida huacha ngozi iliyochanika, na iliyo raruliwa kwa makali
Kuumwa na paka ni majeraha ya ndani ya kutobolewa ambayo mara nyingi hupata maambukizi
Kuumwa na wanyama pori na wanyama wa nyumbani (kama farasi, ng'ombe, na nguruwe) ni nadra. Kuumwa na wanyama wakubwa kunaweza kukuumiza sana. Kuumwa na wanyama wadogo kunaweza kukupa maambukizi.
Je, nipaswa kufanya nini nikiumwa na mnyama?
Unapaswa kutunza jeraha lako na kisha utafute usaidizi:
Safisha jeraha lako kwa sabuni na maji
Usiweke pombe, iodini, au aina nyingine yoyote ya dawa za kuua viini kwenye jeraha lako
Hakikisha kuwa kidonda hakivuji—finya kidonda chako kwa kitambaa safi
Nenda kwa daktari mara moja
Je, kuumwa na wanyama husababisha matatizo gani?
Vidonda vinavyotokana na kuumwa na wanyama vinaweza kuambukizwa
Kidonda kilichoambukizwa ni uchungu, huvimba, na kuwa na wekundu
Ni nadra sana kuambukizwa kichaa cha mbwa kutokana na kuumwa na wanyama fulani
Kichaa cha mbwa ni virusi hatari unavyoweza kupata kutokana na kuumwa na mnyama. Mnyama lazima awe na kichaa cha mbwa kabla ya kukupa kichaa cha mbwa. Sio wanyama wote wanaoweza kupata kichaa cha mbwa.
Nchini Marekani, wanyama kipenzi kwa kawaida huchanjwa dhidi ya kichaa cha mbwa, kwa hivyo ugonjwa huo ni nadra miongoni mwa wanyama hao. Kichaa cha mbwa kinaweza kutokea kwa wanyama fulani wa mwituni, kama vile popo, rakuni, nyegere, au mbweha. Kichaa cha mbwa mara nyingi hakitokani na kuumwa na sungura, kindi, buku, panya, na fuko.
Ikiwa umeumwa na mnyama, unapaswa kumpigia simu daktari wako au uende hospitalini mara moja. Daktari atabaini ikiwa unahitaji chanjo ya kichaa cha mbwa.
Je, madaktari hutibu aje kuumwa kwa mnyama?
Madaktari watafanya:
Kuosha sehemu ya ndani ya jeraha kwa chumvi isiyo na viini (maji ya chumvi yasiyo na viini)
Kukata ngozi yoyote iliyoraruka kutoka kwenye ukingo wa jeraha
Kufunga jeraha kwa kushona, ikiwa inahitajika
Kukupa dawa ili kuzuia maambukizi
Kukupa chanjo ya pepopunda, ikiwa itahitajika
Je, ninawezaje kuzuia kuumwa na mbwa?
Usiache kamwe mtoto au mtoto mchanga peke yake na mbwa
Usisumbue mbwa wakati wanakula au kupumzika
Omba ruhusa kutoka kwa mmiliki wa mbwa kabla ya kushika mbwa
Tulia ikiwa mbwa anakujia, na unyamaze au urudi nyuma polepole
Usijaribu kutenganisha mbwa wanaopigana