Epiglotitisi ni nini?
Kimio chako ni upindo wa tishu kwenye koo lako chini ya ulimi wako. Kinasaidia kuzuia chakula kisiingie kwenye koo la hewa unapomeza. Ikiwa kimio chako kitavimba, inaweza kuziba koo lako la hewa hivyo huwezi kupumua.
Epiglotitisi ni maambukizi ya bakteria kwenye kimio chako.
Dalili kuu zaidi za epiglotitisi na vidonda vikali vya kwenye koo na kalele na kupumua kwa shinda
Epiglotitisi unahatarisha maisha, kwa sababu hutaweza kupumua ikiwa koo lako la hewa litazibwa
Epiglotitisi ni hatari sana kwa watoto kwa sababu wana koo dogo la hewa ambalo linaweza kuzuiwa kwa haraka
Madaktari wanatibu epiglotitisi kwa kutumia dawa za kuua bakteria na kwa kawaida wanaweka neli ya kupumulia kwenye koo la hewa ili lisivimbe na kufunga
Ili kusaidia kuzuia epiglotitisi, mpeleke mtoto wako apate chanjo ya Hib—madaktari wanawapa watoto kama sehemu ya chanjo wanazopaswa kupewa
Watoto na watu wazima ambao wanaweza kuwa na epiglotitisi wanapaswa kwenda haraka kwenye kitengo cha dharura hospitalini.
Nini kinasababisha epiglotitisi?
Epiglotitisi inatokea pale ambapo kimio chako kimeambukizwa bakteria.
Maambukizi hayo yanasababisha kimio chako kuvimba. Hali hii inaweza kuziba njia za hewa hivyo huwezi kupumua.
Dalili za epiglotitisi ni zipi?
Dalili za epiglotitisi zinaaza haraka, hasa kwa watoto. Koo la hewa la mtoto linaweza kuziba ndani ya saa chache baada ya dalili kuanza.
Epiglotitisi mara nyingi ni dharura ya kutishia maisha, kwa hivyo mpeleke mtoto au mtu mzima mwenye dalili hizo hospitalini kwenye kitengo cha dharura.
Watoto wanaweza kuwa na:
Maumivu makali ya koo
Matatizo kumeza vyakula
Homa
Kutokwa mate
Sauti isiyosikika vizuri
Kelele nyembamba wakati wa kuvuta hewa (ukelele), unaosababishwa na kufungwa njia ya hewa
Kupumua kwa shida
Kwa watu wazima, dalili zinafanana na zile za watoto, kwa kawaida zinachukua saa 24 kuonekana. Epiglotitisi inaweza kuziba njia ya hewa ya mtu mzima, lakini hali hii si kubwa sana ikilinganishwa na kwa watoto.
Madaktari wanawezaje kujua kama nina epiglotitisi?
Madaktari wanashuku uwepo wa ugonjwa wa epiglotitisi kulingana na dalili ulizonazo. Ili wawe na uhakika:
Wanaangalia koo kwa kutumia kifaa kinachonyumbuka
Kwa watoto, madaktari wanafanya hivi kwenye chumba cha upasuaji ili wawe tayari kuweka neli ya kupumulia ikiwa inahitajika. Watu wazima kwa kawaida wanaweza kuwa macho na ganzi ikawekwa tu kwenye koo lao.
Je, madaktari wanatibu vipi epiglotitisi?
Jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha kwamba mtu huyo anaweza kupumua.
Kwa watoto:
Madaktari wanaweka neli ya kupumulia kwenye koo la hewa ili njia ya hewa lisivimbe na kufunga
Ikiwa madaktari hawawezi kuweka bomba la kupumulia kwa sababu kimio kinaziba bomba la hewa, watakata tundu mbele ya shingo ili kuweka bomba moja kwa moja kwenye bomba la hewa (tracheostomia)
Mara nyingi, watu wazima hawahitaji neli ya kupumulia, lakini wengine wanahitaji. Utahitaji kubaki hospitalini ili madaktari waweze kukuangalia kwa ukaribu.
Watu wote wenye epiglotitisi wanahitaji dawa za kuua bakteria kupitia mshipa (IV) ili kutibu maambukizi.