Ugonjwa wa Meniere

Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023

Ugonjwa wa meniere ni nini?

Ugonjwa wa Meniere ni tatizo kwenye sikio lako la ndani ambao unasababisha viopindi vya kizunguzungu kikali, kupoteza uwezo wa kusikia na mlio katika sikio lako moja.

  • Dalili zinatokea kwa ghafula na unaweza kuhisi kichefuchefu na kutapika

  • Shambulizi la kizunguzungu kwa kawaida kinadumu kwa saa 1 hadi 6 lakini wakati mwingine linadumu hadi saa 24

  • Ugonjwa wa Meniere unaathiri sikio moja tu

  • Ugonjwa wa Meniere kwa kawaida unatokea kwa watu wenye umri wa miaka 20 hadi 50

  • Mashambulizi kwa kawaida yanakuja na kuondoka

  • Hatimaye unaweza kupoteza uwezo wako wa kusikia kwa kiasi au wote kwenye sikio lililoathiriwa

Ni nini husababisha ugonjwa wa Meniere?

Wakati mwingine ugonjwa wa Meniere unarithishwa kwenye familia. Baadhi ya madaktari wanadhani inaweza kusababishwa na mzunguko hafifu au matatizo kwenye mfumo wa kingamaradhi.

Dalili za ugonjwa wa Meniere ni zipi?

Dalili za kawaida ni:

  • Kizunguzungu kikali ambacho kinakuja ghafula kwa sababu isiyo dhahiri na kinadumu kwa saa kadhaa

  • Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika

  • Mlio kwenye sikio moja tu (kusikia kelele masikioni)

  • Kupungua uwezo wa kusikia kwenye sikio moja

Kizunguzungu hakiwi kibaya au kupata unafuu unapozunguka.

Huenda pia:

  • Kuhisi kujaa au shinikizo kwenye sikio lako, wakati mwingine kabla ya kupata kizunguzungu

Madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa Meniere?

Madaktari wanashuku kuwa una ugonjwa wa Meniere kulingana na dalili ulizo nazo.

Hakuna kipimo ambacho kinaweza kuonyehsa kwa uhakika kwamba una ugonjwa wa Meniere. Lakini wakati mwingine madaktari wanafanya kipimo cha MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ili kuwa na uhakika kuwa si kitu kingine kinachosababisha dalili ulizonazo. Kwa kawaida utafanyiwa kipimo cha uwezo wa kusikia.

Je, madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa Meniere?

Kwa kawaida madaktari watakupa dawa za kutibu kizunguzungu, kichefuchefu na kutapika. Wanakushauri usishiriki kwenye shughuli zozote zinazoongeza hatari ya kuanguka.

Ili kupunguza idadi ya mashambulizi, madaktari wanaweza kupendekeza mambo haya kwenye mlo wako:

  • Chumvi kidogo

  • Usitumie pombe

  • Hakuna kafeini

Daktari anaweza pia:

  • Watakupa diuretic (dawa ambayo inakufanya ukojoe zaidi)

  • Wkati mwingine, watakupa kotikosteroidi kama kidonge au sindano

Madaktari hawawezi kuzuia uwezo wako wa kusikia usiwe na hali mbaya kadiri muda unavyokwenda. Unaweza kuhitaji kisaidizi cha kusikia.

Ikiwa una kizunguzungu kikali na dawa haisaidii, madaktari wanaweza:

  • Kufanya upasuaji ili kutoa baadhi ya majimaji kwenye sikio lako la ndani

  • Kudunga dawa kwenye ngoma ya sikio lako

  • Kama suluhisho la mwisho, kukata neva kwenye sikio lako zinazodhibiti msawazo