Kizunguzungu Chenye Nafuu Kinachotokana na Mwelekeo wa Muda Mfupi

Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023

Kizunguzungu cha kawaida kinachosababishwa na kichwa kusogea ni nini?

Kizunguzungu cha kawaida kinachosababishwa na kichwa kusogea (BPPV) ni aina ya kizunguzungu ambapo unahisi kama unazunguka. Si kibaya sana na kinaisha chenyewe, lakini kinaweza kufanya usijisikie vizuri. Aina hii ya kizunguzungu kinakuja ghafla unapotembea kwa namna fulani.

  • Unapata vipindi vya ghafula ambapo unahisi kama unazunguka na kuhisi kichefuchefu na unaweza kutapika

  • Vipindi hivi huchochewa pale unaposogeza kichwa chako

  • Kwa kawaida hali hii inaisha chini ya dakika moja

  • BPPV inapatikana sana kwa watu wenye umri mkubwa, inaweza kuathiri msawazo na kufanya uwe kama unataka kuanguka

  • Seti ya mwendo inayoitwa mbinu ya Epley huzuia kizunguzungu kwa watu wengi

Ni nini kinachosababisha BPPV?

BPPV hutokea kwa sababu kuna tatizo ndani ya sikio lako ambapo msawazo wako unadhibitiwa. Dutu ndogo za kalisiamu ndani ya sikio la ndani zinalegea na kuelea mahali ambapo si sehemu yake. Hali hii inasababisha dalili zionekane.

Dutu hizi zinahama unaposogeza kichwa chako kwa namna fulani, kama vile:

  • Kujibiringisha kwenye kitanda

  • Kuinama ili kuokota kitu

BPPV inapatikana sana kwa watu wenye umri mkubwa na wanawake.

Dalili za BPPV ni zipi?

Dalili zinakuja kwa ghafula unaposogeza kichwa chako. Dalili za BPPV ni:

  • Vipindi vifupi vya kizunguzungu (vertigo)—unaweza kuhisi kama ama wewe au mazingira yanayokuzunguka yanasonga au yanazunguka

  • Kuhisi mgonjwa tumboni

  • Kutapika

Dalili zake si nzuri lakini si hatari. Hata hivyo, unaweza kupoteza msawazo wako na kuanguka ikiwa utapata kipindi cha BPPV wakati umesimama au unatembea

Madaktari wanawezaje kujua kama nina BPPV?

Madaktari wanatambua ugonjwa wa BPPV kulingana na dalili ulizo nazo na uchunguzi wa mwili. Wanaweza kufanya vipimo vingine kama vile MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku), ikiwa wanahitaji kuhakikisha hupati kizunguzungu kwa sababu nyinginezo ambazo ni hatari zaidi.

Je, madaktari wanatibu vipi BPPV?

Madaktari kwa kawaida wanatibu BPPV kwa kutumia mbinu ya Epley. Mbinu hii ni namna ya kipekee ya kusongesha kichwa na mwili wako. Inahamisha dutu zilizolegea kwenda kwenye sehemu tofuati ya sikio lako ili zisisababishe matatizo.

Mbinu ya Epley: Matibabu ya Kawaida kwa Kisababishi Kikuu cha Kizunguzungu

Mbinu hii inafanywa kwa kufuata mpangilio wa kwenda kulia wa mshale mwekundu hapa chini.

Ili kufanya mbinu ya Epley fanya yafuatayo na ushikilie kila sehemu kwa karibu sekunde 30:

  • Kaa chini kwenye meza au kitanda na ugeuze kichwa chako hadi katikati kuelekea kulia

  • Lala chini kwa mgongo wako huku kichwa chako kikiwa bado kimeelekea kulia na acha kichwa chako kining'inie mwishoni mwa meza au kitanda

  • Geuza kichwa chako upande wa kushoto

  • Sasa geuza kichwa na mwili wako upande wa kushoto pua yako ikiangalia sakafuni

  • Kaa chini taratibu, lakini wakati huo geuza kichwa chako upande wa kushoto

  • Mara unapokuwa umekaa, geuza kichwa chako kitazame mbele

Dalili za BPPV kwa kawaida zinaisha baada ya miezi kadhaa.

Wakati mwingine madaktari wanakupa dawa ili kupunguza kizunguzungu na hali ya kuhisi kichefuchefu, lakini hizi zinaweza tu kusaidia kwa muda mfupi.