Kifaduro ni nini?
Kifaduro ni kuvimba kwenye bomba la pumzi na kisanduku cha sauti. Husababishwa na maambukizi ya virusi na hutokea zaidi kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 3.
Mtoto mwenye kifaduro hupata kikohozi ambacho kinasikika kama kubweka kwa sili
Mtoto anaweza kutoa kelele kubwa wakati anavuta pumzi (kelele ya kukorota) na kuwa na homa na makamasi kwenye pua.
Watoto wengi hupata nafuu nyumbani baada ya siku 3 hadi 4, lakini wengine huhitaji kulazwa hospitalini
Mpigie simu daktari wa mtoto wako mara moja ikiwa mtoto wako ana matatizo ya kupumua.
Mtoto wangu anapaswa kwenda kwa daktari kwa sababu ya kifaduro?
Mpigie simu daktari wa mtoto wako mara moja ikiwa mtoto wako ana mojawapo ya ishara hizi za onyo:
Kupumua kwa shida
Mapigo ya moyo ya haraka
Midomo au vidole vya buluu (kutokana na viwango cya chini vya oksijeni katika damu)
Uchovu usio wa kawaida
Ni nini husababisha kifaduro?
Kifaduro husababishwa na virusi kadhaa tofauti. Mtoto wako anaweza kupata kifaduro wakati wowote wa mwaka, lakini kifaduro hutokea sana katika majira ya joto.
Dalili za kifaduro ni gani?
Dalili za kifaduro mara nyingi huwa mbaya zaidi usiku na zinaweza hata kumwamsha mtoto wako.
Mwanzoni, mtoto wako hupata dalili za baridi kama vile:
Pua zinazotoa kamasi
Kupiga chafya
Kikohozi kidogo
Homa kidogo (100° hadi 101° F au 37.8° hadi 38.3° C)
Baadaye, mtoto wako anaweza kupata:
Kikohozi cha mara kwa mara ambacho kinasikika kama kubweka kwa sili
Baada ya siku 3 hadi 4, kikohozi kinaweza kubadilika na kuonekana kama kikohozi cha kawaida.
Katika kifaduro kikali, mtoto wako pia anaweza kuwa na:
Kupumua kwa shida
Sauti kubwa ya mlio wakati wa anavuta pumzi (kukorota)
Wakati mwingine, rangi ya buluu kwenye midomo kutokana kwa kiwango cha chini cha oksijeni kwenye damu
Madaktari wanaweza kujua vipi ikiwa mtoto wangu ana kifaduro?
Madaktari wanaweza kujua ikiwa mtoto wako ana kifaduro kulingana na dalili za mtoto, hasa sauti ya kubweka anapokohoa. Madaktari watafanya:
Wakati mwingine, kufanya eksirei ya shingo na kifua cha mtoto wako
Madaktari hutibu vipi kifaduro?
Kwa kifaduro kidogo, madaktari watamtibu mtoto wako nyumbani kwa:
Kupumzika
Viowevu visafi kama vile maji au juisi
Kinyunyizio cha unyevu wa ukungu baridi ili kulainisha hewa
Ili kusaidia kupunguza kikohozi, watajaribu mojawapo kati ya yafuatayo:
Kufungulia maji ya moto bafuni ili kuunda mvuke ambao mtoto wako anaweza kupumua
Kumpeleka mtoto wako nje ili apumue hewa baridi ya usiku
Kumwambia mtoto wako apumue hewa baridi kutoka kwenye friza iliyo wazi
Watoto wengi walio na kifaduro kidogo watajisikia vizuri baada ya siku 3 hadi 4.
Ikiwa mtoto wako ana matatizo ya kupumua, nenda kwa idara ya dharura ya hospitali mara moja. Huko, madaktari watampa mtoto wako viowevu kupitia mshipa na dawa kama vile:
Kotikosteroidi kupitia mdomo au sindano
Epinefrini kupitia nebuliza
Nebuliza ni mashine inayotumia umeme au betri inayogeuza dawa ya kiowevu kuwa ukungu ambao mtoto wako anaweza kupumua kwa urahisi kupitia barakoa.
Ikiwa maumivu ya mtoto wako hayapungui, madaktari wanaweza:
Ikiwa mtoto wako bado ana shida ya kupumua, madaktari watamlaza mtoto wako hospitalini. Kawaida madaktari wataendelea:
Kupima kiwango cha oksijeni katika damu ya mtoto wako kwa kuweka kitambuzi kwenye kidole (upimaji wa oksijeni)
Kumpa oksijeni ya ziada kupitia barakoa ikiwa kiwango cha oksijeni cha mtoto wako ni cha chini sana
Kuendelea kutoa dawa kwa nebuliza na kwa mshipa