Haimofilia ni nini?
Haimofilia ni ugonjwa wa kurithi ambapo damu yako haigandi kawaida.
Haimofilia hukufanya utokwe na damu nyingi kutokana na majeraha madogo au hata bila kuumia
Karibu kila mtu aliye na haimofilia ni mwanamume
Wavulana hurithi haimofilia kutoka kwa mama yao
Watu wenye haimofilia hawawezi kutengeneza kipengele cha kutosha cha kuganda (protini zinazosaidia damu kuganda)
Madaktari hutambua uwepo wa ugonjwa wa haimofilia kwa kufanya kipimo cha damu
Unaweza kupata sindano za kipengele cha kuganda kwenye mishipa yako (IV)
Ni nini husababisha haimofilia?
Vipengele vya kuganda ni protini katika damu yako ambavyo husaidia kutengeneza mabonge ya damu iliyoganda. Mabonge ya damu iliyoganda huziba mishipa ya damu inayovuja. Kuna vipengele vingi tofauti vya kuganda.
Katika haimofilia, unarithi jeni isiyo ya kawaida hivyo hutengenezi vipengele vya kutosha vya kugandisha damu
Kuna aina 2 za haimofilia, A na B, kutegemea na kipengele cha kuganda kinachopungua
Jeni zisizo za kawaida zinazosababisha haimofilia hupitishwa kutoka kwa mama yako (zinazohusishwa na ngono).
Haimofilia sio kali kwa kila mtu aliye nayo. Watu wengine hutengeneza kipengele kidogo sana cha kuganda damu kilichoathiriwa. Watu wengine hutengeneza baadhi ya vipengele vya kuganda lakini havitoshi kabisa. Kadiri unavyokuwa na vipengele vichache vya kuganda ndivyo unavyokuwa na uwezekano mbaya zaidi wa kutokwa na damu.
Dalili za Haimofilia ni zipi?
Dalili kuu ya Haimofilia ni:
Unaweza kutokwa na damu kutoka nje, kama vile kutoka kwenye jeraha au pua. Au unaweza kutokwa na damu ndani ya mwili. Kwa mfano, ukipinda goti lako au kugonga mguu wako, unaweza kuvimba ukiwa na damu.
Kwa sababu watu wenye haimofilia wanazaliwa nayo, kwa kawaida matatizo ya kuganda kwa damu huonekana kwa watoto wadogo isipokuwa kama tatizo ni dogo sana.
Unavyotokwa na damu hutegemea jinsi haimofilia yako ilivyo mabaya.
Ikiwa una haimofilia kidogo, unaweza:
Kutokwa na damu nyingi kuliko kawaida, lakini tu baada ya upasuaji, huduma za meno au jeraha
Kutotambulika kamwe
Ikiwa una haimofilia ya wastani, unaweza:
Kutokwa na damu bila jeraha lolote dhahiri wakati mwingine
Wakati wa upasuaji au baada ya kupata jeraha, kutokwa na damu nyingi ambayo ni vigumu kuidhibiti na inaweza kusababisha kifo
Ikiwa una haimofilia mbaya, unaweza:
Mara nyingi kutokwa na damu nyingi baada ya kupata jeraha dogo au bila sababu iliyo dhahiri
Kutokwa na damu nyingi kwenye ubongo wako kutokana na kugongwa kidogo kichwani, hivyo kusababisha uharibifu wa ubongo au kifo
Kutokwa na damu ndani ya kiungo kile kile kunaweza kusababisha ulemavu wa uharibifu wa kiungo.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina haimofilia?
Madaktari wanashuku haimofilia kwa mtoto (hasa mvulana) ambaye huvuja damu nyingi na michubuko kwa urahisi, ikiwa mtoto ana wanafamilia walio na haimofilia.
Ili kugundua ugonjwa wa haimofilia, madaktari hufanya vipimo vya damu ili kuona ikiwa damu yako inaganda kwa kasi ya kawaida na ikiwa kuna vipengele vya kutosha vya kuganda.
Upimaji wa jenetiki unaweza kuonyesha kama mwanamke ni mbeba jeni zisizo za kawaida zinazosababisha haimofilia. Wanawake wajawazito wenye jeni hizi wanaweza kupimwa mtoto wao wakati wa ujauzito.
Madaktari hutibuje haimofilia?
Ikiwa una haimofilia, madaktari wanaweza:
Kuongeza vipengele vya kuganda ili kusaidia damu yako kuganda
Kukupatia dawa ili kupunguza kuvuja damu
Daktari pia atakuekeleza:
Kuepuka hali zinazoweza kukusababishia kuumia na kuvuja damu
Kuepuka dawa, kama vile aspirini, ambazo zinaweza kufanya kuvuja damu kuwa kubaya zaidi
Kutunza vizuri meno na mdomo wako ili using'olewe meno