Anemia ya Upungufu wa Madini ya Chuma

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2022

Anemia ya upungufu wa madini ya chuma ni nini?

Upungufu wa madini chuma ni kuwa na madini chuma kidogo sana mwilini mwako. Madini chuma yapo kwenye seli nyekundu za damu.

Anemia ni hali ya seli za damu kuwa chini. Kwa umahususi, huna seli nyekundu za damu za kutosha.

Unahitaji madini chuma kutengeneza hemoglobini, dutu iliyo kwenye seli nyekundu za damu ambayo inabeba oksijeni kupeleka kwenye mwili wako.

Wakati hakuna madini chuma ya kutosha kwenye mwili wako ili kutengeneza hemoglobini, mwili wako unatengeneza seli nyekundu za damu chache sana. Seli ambazo zinatengenezwa huwa zinakuwa ndogo kuliko kawaida.

  • Anemia ya upungufu wa madini ya chuma ni anemia ambayo hutokea sana

  • Unaweza kuonekana umesawijika na kuhisi mdhaifu na kukosa pumzi

  • Sababu kubwa zaidi ya madini chuma kuwa chini ni kuvuja damu

  • Madaktari wanapima viwango vyako vya madini chuma kwa kutumia vipimo vya damu

  • Madaktari hutibu anemia ya upungufu wa madini ya chuma kwa kutumia vidonge vya madini chuma au kwa nadra madini chuma huingizwa mwilini kupitia mishipa (IV)

Anemia ya upungufu wa madini ya chuma husababishwa na nini?

Sababu kuu za anemia ya upungufu wa madini ya chuma ni:

  • Kuvuja Damu

  • Ongeeko la hitaji la madini chuma mwili unapokua

Unahitaji tu madini chuma kidogo kwenye mlo wako wa kila siku. Hiyo ni kwa sababu mwili wako unatumia tena madini chuma kutoka kwenye seli nyekundu za damu za zamani ili kutengeneza seli nyekundu za damu mpya. Hata hivyo, kuvuja damu kunasababisha mwili wako kupoteza madini chuma. Kuvuja damu ni sababu kuu ya kiwango cha chini cha madini ya chuma na anemia ya upungufu wa madini chuma. Sababu kuu za kuvuja damu hutofautiana kulingana na jinsi na umri:

Katika vipindi vya ukuaji, kama vile ujauzito na utotoni, mwili wako unahitaji madini chuma ya ziada. Ili kuepuka upungufu wa madini chuma katika nyakati hizi unapaswa kula vyakule vyenye madini chuma mengi kama vile nyama, kuku na samaki.

Dalili za anemia ya upungufu wa madini ya chuma ni zipi?

Kwa kawaida dalili zinakuwa mbaya kidogokidogo na hujumuisha:

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Kuonekana umesawijika

  • Kukiwa na madini chuma kidogo sana, dalili za pika (kutaka kula kitu ambacho si chakula, kama vile barafu, uchafu, rangi au chaki)

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina anemia ya upungufu wa madini ya chuma?

Madaktari watafanya vipimo vya damu ili kuangalia kama kuna idadi ndogo ya seli nyekundu za damu (anemia) na kupima viwango vyako vya madini chuma.

Madaktari wanatibu vipi anemia ya upungufu wa madini ya chuma?

Madaktari watafanya:

  • Wanatibu tatizo lolote linalosababisha kuvuja damu

  • Wanahakikisha chakula chako kinajumuisha vyakula vyenye madini chuma mengi

  • Watakuandikia vidonge vya madini chuma (au viowevu kwa watoto)

Ni nadra sana madaktari kutoa madini chuma kuptia mishipa, lakini kwa kawaida hatua hii si lazima.

Kutibu anemia kwa kutumia madini chuma kwa kawaida huchukua wiki 3 hadi 6 kuweza kufanya kazi. Hata hivyo, kwa kawaida utaendelea kutumia madini chuma kwa karibu miezi 6 ili kurejesha madini chuma yote yaliyopotea.

Vidonge vya madini chuma au kiowevu hufanya kazi vizuri ikiwa utavitumia:

  • Asubuhi kabla ya kula

  • Pamoja na sharubati ya machungwa au vitamini C

Madaktari watafanya vipimo vya damu ili kuhaikisha kuwa una madini chuma ya kutosha.