Ujauzito ni kipindi cha kufurahisha ambacho huleta mabadiliko mengi kwa afya ya mama anayatarajia kupata mtoto. Hali hii ya kuvutia pia inaweza kuambatana na msongo wa mawazo. Akina mama na wazazi watarajiwa wanapaswa kuwa kufuatilia kwa ukaribu mabadiliko ya afya ya mama au mtoto.
Hali moja ambayo wazazi wengi watarajiwa wana maswali kuhusiana nayo ni preklampsia. Preklampsia ama shinikizo la juu la damu jipya au hali mbaya zaidi iliyopo ya shinikizo la juu la damu ambayo inatokea baada ya wiki ya 20 ya ujauzito na inaambatana na protini kupita kiasi kwenye mkojo.
Preklampsia inaweza kusababisha kondo kujitenga na/au mtoto kuzaliwa mapema sana, likiongeza hatari ya kwamba mtoto atakuwa na matatizo mara baada ya kuzaliwa. Katika baadhi ya visa, preklampsia inaweza kusababisha kwa ghafla kifafa (eklampsia). Isipotibiwa vizuri, eklampsia kwa kawaida husababisha kifo. Ni muhimu kwa wagonjwa kujiandaa kujadili preklampsia na madaktari wao na kujua dalili za preklampsia. Haya ni majibu ya maswali yanayoulizwa sana na wagonjwa kuhusu preklampsia
1. Je, kuna tofuati gani kati ya preklampsia na shinikizo la juu la damu?
Tofuati kati ya preklampsia na haipatensheni sugu (shinikizo la juu la damu) ni suala la wakati. Baada ya wiki ya 20 ya ujauzito, kuanza kwa shinikizo la juu la damu likiambatana na ongezeko la protini kwenye mkojo hubainishwa kama preklampsia. Kabla ya wiki 20, vipimo vya mwanamke mwenye shinikizo la juu la damu vinaweza kutambuliwa kuwa ana haipatensheni sugu (shinikizo la juu la damu lisilohusiana na ujauzito).
Wanawake wenye haipatensheni sugu, iwe imetambuliwa kabla au wakati wa ujauzito wapo katika hatari ya juu zaidi ya kupata preklampsia. Wanawake wenye haipatensheni sugu kabla ya ujauzito ambao hupata shinikizo la juu la damu linalozidi kuwa baya wanatambuliwa kuwa na kile kinachojulikana kama preklampsia iliyoongezwa juu ya haipatensheni sugu.
2. Ni nani aliye katika hatari ya kupata preklampsia?
Preklampsia inaweza kutokea kwa mwanamke yeyote mjamzito. Hata akina mama watarajiwa ambao hawana matatizo ya afya hapo awali wanaweza kuwa katika hatari. Kwa hivyo, preklampsia huwapata sana wanawake wenye matatizo au sifa fulani, ikiwa ni pamoja na shinikizo la juu la damu kabla ya ujauzito.
Hatari zingine zinajumuisha preklampsia katika ujauzito uliopita, kisukari kabla ya ujauzito (kisukari aina ya 1 au ya 2) au kilichotokea wakati wa ujauzito (kisukari wakati wa ujauzito), uzito kupita kiasi, kubeba mimba katika umri mkubwa (zaidi ya miaka 35) au umri mdogo (chini ya miaka 18), na ndugu ambao wamewahi kuwa na preklampsia. Wanawake waliopata ujauzito kupitia urutubishaji wa mbegu au wenye ugonjwa wa kingamwili kwenda kinyume na mwili wanaweza pia kuwa katika hatari kubwa.
3. Je, ishara na dalili za preklampsia ni zipi?
Kufuatilia dalili za kawaida za preklampsia ni muhimu sana kwa ujauzito, kujifungua na kipindi cha baada ya kujifungua chenye afya. Dalili ya kawaida ya kuangalia baada ya wiki 20 ni maumivu ya kichwa ambayo hayaishi. Mabadiliko katika uwezo wa kuona kama vile ukungu, nuru ya kumulika ghafla, madoa au kudhuriwa na mwanga kwa urahisi pia inaweza kuwa dalili. Baadhi ya akina mama wanaotarajia kupata watoto hupata kichefuchefu katika kipindi chote cha ujauzito. Lakini kichefuchefu kipya au hali ya kutapika ambayo hutokea baada ya wiki ya 20 inaweza kuwa ishara ya preklampsia. Mambo mengine ya kuangalia hujumuisha maumivu upande wa juu kulia ambao ni mojawapo ya pande nne za sehemu ya katikati na kuvimba uso, mikono, vidole, shingo na/au miguu.
Mwanamke mjamzito anapaswa kumpigia simu daktari wake ikiwa anahisi maumivu mapya ya kichwa ambayo hayaishi au kupungua kwa kutumia acetaminophen au ikiwa ana uvimbe wa ghafla kwenye mikono au uso. Ukiwa na wasiwasi, wasiliana na daktari—ni muhimu kuhakikisha iwapo kuna tatizo la kiafya.
4. Je, preklampsia inaweza kusababishwa na haipatensheni ya muda mfupi isiyokuwa na madhara?
"Haipatensheni ya muda mfupi isiyokuwa na madhara" ni neno la kawaida kwa watu ambao hupata shinikizo la juu la damu katika mazingira ya kitabibu lakini si katika maisha yao ya kila siku. Wanawake ambao wanapitia wasiwasi wakati wa vipimo vya shinikizo la damu wakati wa miadi ya kitabibu wanapaswa kuzungumza na madaktari wao kuhusu suala hili. Hata hivyo, ikiwa vipimo vya shinikizo la damu viko juu, kwa kawaida hurudiwa. Ikiwa bado vipo juu, hii kwa kawaida inamaanisha kwamba huenda kuna tatizo ambalo linapaswa kufuatiliwa na kuchunguzwa kuona iwapo matibabu yanahitajika. Matokeo yote ya shinikizo la juu la damu yanayolingana yanahitaji kushughulikiwa na kuchukuliwa kwa uthabiti, haswa wakati wa ujauzito.
5. Je, preklampsia hutibiwa vipi?
Kutibu preklampsia si kama kutibu shinikizo la juu la damu sugu. Wanawake wenye preklampsia au eklampsia kali mara nyingi hulazwa hospitalini katika uangalizi maalumu au katika hali fulani, kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Katika wiki 37 na zaidi, mara nyingi kujifungua ndiyo "tiba" ya preklampsia.
6. Je, preklampsia inaweza kuzuiwa?
Linapokuja suala la kuzuia na kutibu preklampsia, kuna dhana potofu kadhaa za kawaida ambazo zinapaswa kushughulikiwa. Mlo usiokuwa na chumvi na kupumzika kitandani hakutazuia au kutibu preklampsia. Wala kupunguza msongo wa akili na mwili (ingawa hizi ni njia nzuri wakati wowote na hasa wakati wa ujauzito).
Kwa baadhi ya wanawake walio katika hatari ya juu, madaktari wanaweza kutoa dozi ya chini ya aspirini itakayotumiwa kila siku katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza. Tafiti zimeonyesha kwamba hii inapunguza hatari ya kutokea preklampsia. Aidha, ni muhimu kuchukua hatua ili kuwa mwenye afya kadiri iwezekanavyo na kudhibiti matatizo yoyote sugu kabla ya kupata ujauzito.
7. Je, wajawazito wenye preklampsia wanapaswa kujifungua kwa njia ya upasuaji wa kupasua tumbo la uzazi?
Wanawake wengi walio na preklampsia wanaweza kujifungua kwa njia ya kawaida. Kuwa na preklampsia hakumaanishi kuwa mwanamke anapaswa kujifungua kwa njia ya upasuaji wa kupasua tumbo la uzazi. Madaktari wataangalia mambo mengi katika kuamua mchakato wa kujifungua unaopendekezwa. Mwishowe, inategemea ukali wa preklampsia, uimara wa mama na hali ya mtoto.
8. Je, kuna ufuatiliaji upi wa preklampsia baada ya kujifungua?
Baada ya kujifungua, wanawake waliokuwa na preklampsia wanapaswa kumwona daktari wao kwa ajili ya kufanya vipimo vya shinikizo la damu angalau kila baada ya wiki 1 hadi 2 baada ya kujifungua. Pia ni muhimu kuzingatia kwamba preklampsia inaweza kutokea baada ya kujifungua. Ikiwa mwanamke ana dalili za preklampsia katika kipindi cha baada ya kujifungua, anapaswa kumpigia simu daktari wake.
Kwa maelezo zaidi kuhusu preklampsia, tembelea Mada ya Mwongozo au Vidokezo vya Haraka kuhusu mada hii.