Endometriosisi ni nini?
Endometriosisi ni hali inayosababishwa na tishu za endometriamu kukua nje ya uterasi yako, kwa kawaida katika maeneo mengine ndani ya tumbo lako.
Mara nyingi tishu hukua kwenye au nje ya ovari, uterasi, na mirija ya uzazi.
Tishu yoyote ya endometriamu ambayo ipo mahali pasipofaa hufanya kazi kama tishu za endometriamu ndani ya uterasi yako. Inakua kisha inatoka kama damu kila mwezi pamoja na hedhi zako, ambayo inaweza kuwa chungu na inaweza kusababisha tishu yenye kovu kukua. Wakati mwingine tishu yenye kovu huzuia mirija yako ya uzazi, jambo ambalo hufanya iwe vigumu zaidi kupata mimba.
Sababu halisi ya endometriosisi haijulikani.
Unapopata ugonjwa huu wa endometriosisi, vipande vya tishu za endometriamu vinavyopaswa kutoka mwilini pamoja na damu ya hedhi huelekea kwenye mirija ya uzazi. Inawezekana hata chembe hizo ndogo kukwama ndani ya tumbo lako na kuanza kukua.
Wakati mwingine endometriosisi hutokea katika familia.
Maumivu ndiyo dalili inayojitokeza zaidi.
Wanawake tofauti wanaweza kuwa na aina tofauti za maumivu:
Maumivu kwenye tumbo la chini, hasa kabla na wakati wa hedhi
Maumivu wakati wa kufanya ngono
Maumivu unapopitisha kinyesi
Maumivu wakati unakojoa
Ukiwa mjamzito, dalili zinaweza kutoweka kwa muda mfupi au kabisa. Wakati mwingi dalili hutoweka unapofikia kikomo cha hedhi.
Madaktari wanaweza kushuku endometriosisi ikiwa una maumivu ya tumbo ambayo yanaonekana kutokea na kuisha wakati wa hedhi au unapofanya ngono au ikiwa una shida kupata ujauzito.
Ili kuhakikisha kama una endometriosisi, daktari anaweza kuangalia ndani ya tumbo lako kwa kutumia mrija unaonyumbulika wa kutazama. Wakati wa utaratibu huu, utapewa daa ya ganzi na kisha daktari wako ataingiza mrija wa kutazama kupitia mkato mdogo karibu na kitovu.
Matibabu yanategemea dalili, mipango ya ujauzito, umri, na hatua ya endometriosisi.
Madaktari hutibu endometriosisi kwa kutumia dawa ya kupunguza uvimbe isiyo na asteroidi (NSAID) ili kupunguza maumivu, dawa zilizo na homoni (kama vile vidonge vya kudhibiti uzazi), au upasuaji kwa kutumia laparoskopi kuondoa au kuharibu tishu za endometriamu ambazo hazijawekwa sawa.
Hakimiliki © 2023 Merck & Co., Inc., Rahway, NJ, USA na washirika wake. Haki zote zimehifadhiwa.