Kupumua Kwa Shida Wakati wa Kulala
Wakati wa kupumua, mapafu yamejazwa hewa na oksijeni inabadilishwa kwa kaboni dioksidi kwenye alveoli. Kaboni dioksidi unaondoka kwenye mwili wakati wa kupumua. Kwa kawaida, mchakato huu unatokea bila kuingiliwa.
Kupumua kwa shida wakati wa kulala ni tatizo la usingizi ambalo lililoenea sana na lenye sifa ya mtu kusita sita wakati wa kupumua akiwa umelala. Kukoma kupumua, au kipindi cha wakati wambapo kupumua kunaisimama, kwa kawaida hudumu kwa sekunde 10 hadi 20 na huweza kutokea mara 20 hadi 30 kwa saa kila usiku.
Kuna aina tatu za hali ya kupumua kwa shida wakati wa kulala.
Kizuizi kinachosababisha kupumua kwa shida wakati wa kulala
Kupumua kwa shida wakati wa kulala kunakotokana na mfumo wa fahamu
Mchanganyiko wa matatizo ya kupumua kwa shida wakati wa kulala (muunganiko wa yote mawili)
Kizuizi kinachosababisha kupumua kwa shida wakati wa kulala hutokea wakati misuli iliyo nyuma ya koo, inayoshikilia paleti laini inapolegea. Misuli inapostarehe, njia ya hewa inakuwa nyembamba na kupumua kunazuiliwa kwa muda. Hali hii inapunguza kiwango cha oksijeni kwenye damu, ikichochea ubongo kuamsha mwili kutoka usingizini ili kufungua tena njia ya hewa.
Kizuizi kinachosababisha kupumua kwa shida wakati wa kulala ni hali inayowapata sana watu wenye uzani mkubwa kupita kiasi. Dalili za kawaida zinaweza kujumuisha
Usingizi wa mchana kupita kiasi
Kukoroma kwa sauti kukiwa na vipindi vya ukimya kukifuatiwa na kutweta
Usingizi usio na utulivu
Kuamka kinywa kikiwa kikavu au koo lanye maumivu
Mshine za CPAP, matumizi ya vifaa vya kinywani na tiba ya oksijeni ni tiba zilizozoeleka. Katika mazingira fulani, upasuaji unatumika kuondoa uzuiaji unaoziba njia za hewa.
Daktari wako ni chanzo kikubwa cha taarifa kuhusu matibabu. Ni muhimu kujadili na daktari wako ni tiba ipi, ikiwa ipo, inayofaa zaidi.