Kuziba kwa Mishipa ya Mapafu

Mfumo wa mzunguko unabeba damu kwenye mwili wote kupitia mtandao thabiti wa ateri na mishipa. Mfumo wa mishipa ni sehemu ya mfumo wa mzunguko wa damu inayotumia mishipa kurudisha damu iliyotumika au isiyo na oksijeni kwenda kwenye moyo na mapafu.

Mara kwa mara, hali isiyo ya kawaida kwenye ukuta wa mshipa (hasa kwenye maeneo ya mtiririko wa polepole, kama vile eneo linalozunguka valvu za mishipa) inaweza kusababisha damu iliyoganda, mvilio kujiunda. Mara baada ya kujiunda, fibrin na seli nyekundu za damu zinaeza kusababisha mvilio kukua ndani ya mishipa. Pamoja na kusababisha mwako kwenye mshipa na kuzuia damu kutiririka, kuna hatari kubwa kwamba mvilio wa mishipa wote au kwa sehemu unaweza kupasuka na kusafiri kwenye mtiririko wa damu. Mivilio hii inayotembea, au emboli hatimaye inaweza kuingia kwenye mishipa ya damu ya mapafu. Hali iliyotokea ya kuganda damu, inayoitwa kuziba kwa mishipa ya mapafu, huweza kuhatarisha mtiririko wa damu kwenye mapafu na kusababisha kukata pumzi, wepesi wa kichwa, kukohoa, maumivu ya kichwa na hata kupoteza fahamu au kifo.

Ukuaji wa kuziba kwa mishipa ya mapafu ni dharura ya kitabibu ambayo inahitaji kushughulikiwa haraka kitabibu.