Damu Iliyoganda: Kuziba Ulipokatwa

Kuvu damu hutokea wakati kuta za mishipa ya damu zimevunjika. Udhibiti wa kuvuja damu (hemostasisi) huanza wakati chembe sahani katika damu zinapoamilishwa (kubadilisha sura na kuendeleza miiba) na kushikamana na eneo lililojeruhiwa. Chembe sahani hufanya wavu pamoja na seli za damu, kolajeni, na protini nyingine. Nyavu hii, iliyoimarishwa na nyuzi ndefu za fibrini isiyoyeyuka, hunasa chembe sahani na chembe nyingi za damu, na kutoa tone la damu ambalo huziba mwanya huo. Damu iliyoganda huyeyuka mshipa wa damu unapopona.