Mapigo ya Haraka ya Moyo Kwenye Atiria

Moyo ni musuli ambao unabana katika mpangilio wa mdundo kwa muda wa maisha yetu. Kila mdundo unachechemuliwa na ishara ya umeme ambayo inazalishwa na mfumo wa upitishaji wa moyo. Moyo wa kawaida hudunda mara 60 hadi 100 kwa kila dakika. Wakati mwingine, tatizo la mfumo wa upitishaji husababisha moyo kudunda haraka zaidi, polepole zaidi au kuwa na mdundo usio wa kawaida au hakika. Kipimo, kinachoitwa elektokadiogramu, au EKG kinaweza kupima na kurekodi shughuli ya umeme ya moyo.

Katika mdundo wa moyo wa kawaida, ishara ya moyo hufuata njia maalum kupitia kwenye moyo. Ishara huanzia kwenye kifundo cha sinoatria, au nodi ya SA, iliyo kwenye atriamu ya kulia. Nodi ya SA huchochea atiria ili kubana, kusukuma damu kwenye ventrikali. Kisha ishara ya umeme inasafiri kupitia kwenye nodi triskupidia, au nodi ya AV na kwenye ventrikali. Ishara sasa husababisha ventrikali kubana, kupiga damu kwenye mapafu na mwili.

Mapigo ya haraka ya moyo kwenye atiria ni aina ya mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida ambayo yanasababishwa na ishara za umeme zisizo hakika ambazo chanzo chake ni atiria. Katika usumbufu huu wa mdundo, mibano ya kawaida iliyoratibiwa kati ya atiria na ventrikali husumbuliwa, hivyo kuingilia uwezo wa moyo wa kupeleka damu kwa ufanisi kwenye mwili.

Kwa watu ambao wanapata mapigo ya haraka ya moyo kwenye atiria, misukumo mingi ya umeme ya haraka ambayo chanzo chake ni kutoka maeneo tofauti ya moyo yanatumwa kwenye atiria. Misukumo hio husababisha mdundo uliovurugika na wa kasi ya juu. Kwa sababu ya mdundo huu, mibano ya atiria ikawa isio hakika. Kutokana na hilo, mibano isiyo ya kawaida ya atiria haijazi vizuri ventrikali kwa damu, hivyo kusababisha mibano ya ventrikali kuwa isiyo ya hakika pia. Kipimo cha mapigo ya moyo kinaweza kuongezeka kiwe midundo 100 hadi 175 kwa kila dakika au zaidi.

Mapigo ya haraka ya moyo kwenye atiria inaweza kusababisha kuzirai, udhaifu na inaweza kusababisha damu iliyoganda na matatizo mengine. Hali hio inaweza kutibiwa kwa dawa au kwa upasuaji. Kwa baadhi ya wagonjwa, kidhibiti mapigo ya moyo kinaweza kuingizwa ili kudhibiti mdundo wa moyo.